Habari za Punde

TPA YAIPIGA ‘JEKI’ HOSPITAL YA WILAYA, WAVUVI CHATO

 Kaimu Mkurugenzi wa Manunuzi, Mikataba na Ugavi, wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA), Mhandisi Augustino Philipo (wa pili kulia) na Mkuu wa Wilaya ya Chato, Shaaban Ntarambe (kushoto) kwa pamoja na Kaimu Mkuu wa Bandari ya Mwanza, Daniel Sira na Kaimu Mganga Mfawidhi wa Hospital ya Chato Dkt. Eustadius Kwamba (kulia) wakimfunika mmoja wa watoto waliolazwa katika Hospitali ya Wilaya ya Chato jana baada ya TPA kukabidhi msaada wa mashuka 300 kwa ajili ya wodi ya watoto. Mbali na huduma ya afya TPA pia ilitoa msaada wa ujenzi wa Choo na Ofisi ya wavuvi wa Mwalo wa Chato. 
 Kaimu Mkurugenzi wa Manunuzi, Mikataba na Ugavi, wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA), Mhandisi Augustino Philipo (mwenye koti jeusi) akikagua moja ya mashuka 300 ya msaada yaliyotolewa na TPA kwa ajili ya wodi ya watoto ya Hospitali ya Wilaya ya Chato jana, kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Chato, Mkuu wa Wilaya ya Chato, Mhe Shaaban Ntarambe na anayeshudia kushoto ni Kaimu Mkuu wa Bandari ya Mwanza, Bw. Daniel Sira.
Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) imeipiga tafu hospital ya Wilaya Chato kwa kukukabidhi Mashuka 300 kwa ajili ya wodi ya watoto na vifaa vya ujenzi kwa ajili ya kukamilisha ujenzi wa ofisi na choo cha mwalo wa Chato. 
Kaimu Mkurugenzi wa Manunuzi, Mikataba na Ugavi, wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA), Mhandisi Augustino Philipo ambaye alimwakilisha Mkurugnzi Mkuu wa Mamlaka katika hafla hiyo alisema, Mamlaka inatambua na kuthamini kazi kubwa inayofanywa na Serikali hii ya Awamu ya Tano ya Mhe. Dk. John Pombe Joseph Magufuli ya kufikisha huduma mbalimbali za jamii kwa wananchi wa hali ya chini.
Kwa TPA, alisema kwamba inatambua na kuthamini juhudi kubwa inayofanywa na Serikali ya kuhakikisha jamii inapata huduma muhimu, inayo sera ambayo imejikita katika kuisaidia jamii katika nyanja za afya, elimu na maendeleo ya jamii.
“Tunaamini kwamba msaada huu utasaidia kupunguza changamoto za uhaba wa mashuka na vifaa tiba katika hospitali ya Wilaya ya Chato,” alisema Mhandisi Philipo.
Mhandisi Philipo amesema kwamba pamoja na shughuli zetu kubwa za kupakia na kupakua mizigo, Mamlaka pia ina wajibu wa kurudisha kile inachokipata kutokana na huduma zake kwa kuisaidia jamii na ndio maana leo hii tumekuja kutekeleza wajibu huo.
“Kwa kutambua hilo, leo TPA tumefika katika Wilaya hii ya Chato kukukabidhi Mashuka 300 kwa ajili ya wodi ya watoto na vifaa vya ujenzi kwa ajili ya kukamilisha ujenzi wa ofisi na choo cha mwalo wa Chato” amesema.
Amesisitiza tunatambua kwamba ili viongozi wetu wawatumikie ipasavyo wananchi wetu wanapaswa kuwa na mazingira mazuri ya kufanya kazi na ndio maana tukawa tayari kusaidia ujenzi wa ofisi hiyo lakini kubwa zaidi kusaidia jamii ni sehemu na wajibu wa Mamlaka kwa Watanzania. 
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Chato, Mhe Shaaban Ntarambe aliishukuru TPA kwa msaada huo ambao umesaidia kwa kiasi kikubwa kutatua changamoto za uhaba wa mashuka hoapitalini hapo.
Naye Kaimu Mganga Mfawidhi wa Hospital ya Chato Dkt. Eustadius Kweyamba amesema kwamba msaada huo umewasaidia kwa kiasi kikubwa kwani katika hospital hiyo walikuwa na uhaba wa mashuka 453 kati ya 700 yanayohitajika.
“Msaada huu umetuwezesha kuongea idadi ya mashuka tuliyonayo hadi kufikia 524 hivyo tunapenda kutoa wito kwa taasisi nyingine kuiga mfano huu wa TPA katika kusaidia huduma za afya,” alisema.
Mbali na mashuka TPA pia imetoa vifaa vya ujenzi kwa ajili choo na ofisi ya wavuvi katika mwalo wa Chato. Wavuvi hao wanaofikia zaidi ya 2,000 wamekuwa wakifanya kazi zao bila ya kuwa na sehemu maalumu ya kujisaidia.
Wameishukuru TPA kwa msaada huo kwani umewaondolea kero iliyokuwa ikiwasumbua kwa miaka mingi katika Mwalo huo pekee unaotumiwa eneo hilo la Chato pembezi mwa Ziwa Victoria.
Thamani ya msaada huu ni Tshs. Milioni Kumi na Tano (15,000,000/=).

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.