Habari za Punde

TUNDU LISSU AKAMATWA UWANJA WA NDEGE AKIJIANDAA 'KUTIMKIA' RWANDA


Mbunge wa Singida Mashariki (CHADEMA) na Mwenyekiti wa Chama cha Wanasheria cha Tanganyika (TLS) Mhe. Tundu Lissu (pichani) amekamatwa leo, Alhamisi Julai 20 katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) akielekea Kigali, Rwanda kwenye kikao cha chama cha wanasheria cha Afrika Mashariki (EALS)
Kamanda wa polisi viwanja vya ndege Bw, Martn Ortieno amethibitisha kwamba ni kweli wamemkamata Lissu ambaye pia ni Mwanasheria wa Chadema na kwamba amepelekwa makao makuu ya Polisi. Hata hivyo kamanda huyo hakutaja sababu za kukamatwa kwa mwanasheria huyo.
Mkurugenzi wa Itifaki, Mawasiliano na Mambo ya Nje wa CHADEMA Bw. John Mrema naye amethibitisha kuwa mwanasheria huyo amekamatwa jioni hii. 
Mrema amesema Lissu amekamatwa na watu waliojitambulisha kuwa ni maofisa wa polisi 
kutoka Kanda Maalum ya Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.