Habari za Punde

WANANCHI WAIOMBA SERIKALI IONGEZE MUDA ZAIDI WA KULIPA KODI YA MAJENGO

 Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) (kushoto) akiongea na wananchi waliojitokeza kulipa kodi ya majengo katika Ofisi za Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA)-Ilala Mtaa wa Kipata, na kuwapongeza kwa kuitikia wito huo kwa wingi na kuwaeleza kuwa kwa kulipa kodi kutasaidia upatikanaji wa huduma muhimu kama maji, barabara, umeme  na dawa hospitalini.
 Wananchi waliofika katika Ofisi za Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Ilala Mtaa wa Kipata, wakimsikiliza Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb), (kulia) akiwaelezea namna atakavyoboresha huduma kwa walipa kodi za majengo kwa kuwapa kipaumbele walemavu, wazee, wagonjwa na wasiojiweza. Tukio hili litaenda sambamba na kuwawekea sehemu maalumu ya kukaa wakati wakisubiri huduma.
 Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb), (kushoto) akipokea shukrani na pongezi kutoka kwa Bi. Rose Muyalo, kwa utendaji makini wa Serikali ya Awamu ya Tano na kwa kupatiwa huduma bora kutoka kwa wafanyakazi wa TRA.
 Bw. Obedi Hezron Misoji (kulia) ambaye ni mstaafu akimuomba Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) (kushoto), kuongeza muda wa zoezi hili la ulipaji kodi ya majengo kwani watu bado ni wengi na Watanzania wameonesha nia yakujitokeza kwa wingi kulipia kodi hiyo.
 Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb), (kulia) akiongea na wananchi waliofika katika Ofisi za Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Ilala Mtaa wa Kipata kulipa kodi za majengo na kuelezea furaha yake namna walivyoitikia wito huo.
Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) (kushoto), akiwasikiliza viongozi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Ilala Mtaa wa Kipata namna ambavyo wanaweza kukabiliana na changamoto wanazokabiliana nazo katika zoezi hili la ulipaji kodi wa Majengo.  Kutoka kulia ni Meneja Msaidizi Kanda ya Ilala kwa upande wa madeni Bw. Nuhu Ramadhani, Meneja wa Kanda ya Ilala Bw. Abdul Mapembe na Bw. Revelian Kajuna. Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini-WFM

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.