Habari za Punde

WAZIRI MKUU MAJALIWA ASEMA TATIZO LA UMEME LINDI NA MTWARA KUWA HISTORIA, MRADI WA UMEEM WA TANESCO MAHUMBIKA NI MKOMBOZI

NA K-VIS BLOG, Lindi

WAZIRI MKUU Mhe. Kassim Majaliwa ametembelea kituo cha kupoza na kusafirisha umeme kilichoko kijiji cha Mahumbika kilichoko Wilaya ya Lindi na kusema tatizo la kukatika umeme mikoa ya Lindi na Mtwara kumalizika kabisa ujenzi wa kituo hicho utakapokamilika.
Waziri Mkuu ambaye alitembelea mradi huo jioni ya Alhamisi Julai 13, 2017, alisema mradi huo utakapokamilika, uwezo wa kusafirisha umeme utafikia Msongo wa Kilovoti 132, kutoka Msongo wa kilovoti 32 za sasa.
Waziri Mmju alisema azma ya Serikali kupitia Shirika lake la umeme TANESCO ni kuongeza kiwango cha uzalishaji wa umeme kote nchini ili Watanzania wapate umeme mwingi na wa uhakika utakaosambazwa hadi vijijini na kwa gharama nafuu. KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
“Mikoa wa Lindina Mtwara ilikuwa na shida kubwa ya kukatika kwa umeme mara kwa mara mradi huu ni mkombozi kwa wana Lindi na Mtwara, tunawakaribisha wawekezaji waje kuwekeza kwa sababu sasa nishati ya umeme ni ya uhakika.” Alisema Mhe. Majaliwa.

Alisema mradi huo umegharimu kiasi cha Sh. bilioni 16 fedha za walipa kodi wa Tanzania.
Naye Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Profesa James Mdoe amesema mradi huu utawezesha kuimarika kwa upatikanaji wa umeme wa uhakika na hivyo kuwahakikishia Watanzania kuwa safari ya kuelekea ujenzi wa uchumi wa viwanda ni ya uhakika.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akisalimiana na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madini Prof. James Mdoe, wakati alipotembelea mradi wa kuzalisha umeme unaojengwa katika kijiji cha Mahumbika wilayani Lindi, akiwa njiani kuelekea Lindi, Waziri Mkuu yupo Mkoani Lindi kwa ziara ya kikazi ya siku nne (katikati) ni Mbunge wa Jimbo la Mtama Nape Mnauye. 13, 2017. 
Mhe. Waziri Mkuu, akikagua mradi huo wa Mahumbika.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akipokea maelezo ya mradi wa kuzalisha umeme unaojengwa katika kijiji cha Mahumbika wilayani Lindi kutoka kwa Mhandisi Jafary Msuya, wakati alipotembelea mradi huo unaojengwa katika kijiji cha Mahumbika wilayani Lindi, Waziri Mkuu yupo Mkoani Lindi kwa ziara ya kikazi ya siku nne 13, 2017.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akipokea maelezo ya mradi wa kuzalisha umeme unaojengwa katika kijiji cha Mahumbika wilayani Lindi kutoka kwa Mhandisi Ferdinand Mwinje, wakati akikagua mradi huo unaojengwa katika kijiji cha Mahumbika wilayani Lindi, Waziri Mkuu yupo Mkoani Lindi kwa ziara ya kikazi ya siku nne 13, 2017. 
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akiongea na wananchi, wakati alipotembelea mradi wa kuzalisha umeme wa Mahumbika, unaojengwa katika kijiji cha Mahumbika wilayani Lindi, Waziri Mkuu yupo Mkoani Lindi kwa ziara ya kikazi ya siku nne 13, 2017. Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu​

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.