Habari za Punde

WAZIRI MWAKYEMBE AUNDA KAMATI YA KUCHUNGUZA UBIA WA STAR TIMES NA TBC
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo, Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe ameunda Kamati ya kuchunguza ubia wa Kampuni ya StarTimes na Shirika la Utangazaji la Taifa (TBC) kufuatia hoja mbalimbali zilizojitokeza. 
Kamati hiyo iliyoundwa na Waziri Mwakyembe itaongozwa na Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO), Dkt. Hassan Abbasi. 
Kamati hiyo itakuwa na jumla ya Wajumbe 10 watakaochunguza utendaji wa Kampuni ya ubia ya StarTimes, ambapo watano (5) ni wa upande wa Tanzania na wengine watano (5) ni wa kutoka Star Media China. 
Wajumbe wanaounda Kamati hiyo kwa upande wa Tanzania ni kama wafuatao;- 1. Dkt. Hassan Abbasi (Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo) 2. Kyando Evod (Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo) 3. Frederick Ntobi (Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania-TCRA) 4. Eng. James Kisaka (Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania-TCRA) 5. Mbwilo Kitujime (Shirika la Utangazaji la Taifa-TBC) 
Aidha, majina ya Wajumbe watano walioteuliwa kutoka Star Media China yatawasilishwa kutoka China ili kukamilisha idadi kamili ya wajumbe 10 wa kamati hiyo. 
Kamati hiyo imepewa hadidu za rejea takribani nane na inatakiwa kufanya kazi kwa muda wa siku saba ili kukamilisha kazi hiyo. 

Imetolewa na: 
Zawadi Msalla Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo. 15 Julai, 2017.


No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.