Habari za Punde

WAZIRI PROF.MAKAME MBARAWA AFANYA ZIARA UWANJA WA JNIA

Kaimu Mkurugenzi wa Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (TBII-JNIA), Bw. Joseph Nyahende (wa pili kushoto) akitoa ufafanuzi wa namna abiria wenye viza wanavyohudumiwa kwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhe. Prof. Makame Mbarawa (mwenye miwani kifuani). Pembeni ya Waziri ni Katibu Mkuu sekta ya Uchukuzi, Dr. Leonard Chamuriho na nyuma mwenye suti nyeusi ni Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania, Bw. Salim Msangi.
Katibu Mkuu wa chama cha madereva wa taxi wa Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere, Bw. Simon Mwampashi (kulia), akitoa maoni mbalimbali kwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhe. Prof. Makame Mbarawa leo alipofanya ziara JNIA.Mkuu wa Kitengo cha Idara ya Uhamiaji Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere, Bw. Flugence Andrew (kulia) akitoa maelezo ya utaratibu unaotumika kulipia viza kwa Mhe. Makame Mbarawa, Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano leo alipofanya ziara kwenye jengo la abiria la kiwanja hicho. Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhe. Prof. Makame Mbarawa leo akiwa katika mfumo wa kupokelea mizigo kwa abiria wanaowasili kwenye Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere alipofanya ziara ya kutembelea maeneo mbalimbali. Mwenye kizibao ni Kaimu Mkurugenzi wa kiwanja hicho, Bw. Joseph Nyahende.Afisa Forodha Msaidizi, Hezron Giso (kulia), akielezea shughuli anazozifanya ndani ya Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (TBII-JNIA), kwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhe. Prof. Makame Mbarawa (mwenye miwani kifuani), wakati wa ziara ya Waziri iliyofanyika leo.
Prof. Makame Mbarawa, Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano akimsikiliza Kaimu Mkurugenzi wa Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (TBII-JNIA), mwenye kizibao akielezea jambo katika meza ya ukaguzi wa tiketi za abiria wanaosafiri. Kulia ni Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), Bw. Salim Msangi.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.