Habari za Punde

ALAMA HIZI ZA MUDA MREFU BILA KUTUMIKA MITAA YA JIJI LA DAR NI ELIMU INATAKIWA KWA MADEREVA NA SI KUWAADHIBU BILA KUJIPANGA

 Askari wa Usalama Barabarani, Koplo, Ezekiel akizungumza na dereva mwenye gari lenye namba za usajili T 175 BMC aimuelimisha baada ya kumkamata akipita katika barabara ya Makunganya yenye alama inayozuia kupishana magari 'No Entry'  wakati wa Operesheni maalumu ya kuwahiza na kuwataka kutfuata alama za barabarani iliyoanza wiki iliyopita jijini Dar es Salaam.  Picha na Muhidin Sufiani (MAFOTO)
 Swala akikatiza katika msitu huu basi yeye kidume.....
 Askari wa Usalama Barabarani Koplo Ladislaus akisimamisha gari lililokuwa likitokea njia isiyoruhusiwa Barabara ya Makunganya.
 Askari wa Usalama Barabarani, Koplo, Ezekiel (kushoto) na Koplo, Ladislaus, wakimwandikia makosa dereva wa gari ndogo lenye namba za usajili T 698 DHQ aliyepita katika Barabara ya Makunganya Posta jijini Dar es Salaam, ambayo ina kibao cha alama ya kuzuia kupishana magari. Askari wa usalama barabarani wameanza operesheni ya kukamata magari yanayovunja sheria za usalama barabarani na kutumia njia zisizo ruhusiwatoka wiki iliyopita. 
 Dereva akilimwa cheti yaani akikabidhiwa Risiti yake baada ya kuandikiwa kosa na kupigwa faini.
 Weka pembeni.....
 Hii ni moja ya alama za barabarani
 ALama hii ipo sehemu sahihi lakini imefutika wahusika kabla ya kuwaadhibu madereva mjirekebishe na ninyi kwanza
 Dereva huyu wa Premio (kushoto) kama haioni alama hii inayomzuia kwenda.
 Alama hii inaonekana vizuri tu lakini ilipowekwa si sehemu sahihi kwa dereva kugundua inamzuia kwenda na njia hii,kwani imewekwa upande wa kulia huku njia hii ikiwa na matoleo mawili na mzunguko yaani 'Round about'
 Alama hiyo hapo juu ilibidi kuwekwa kushoto kwa dereva wa gari hii ndogo nyeupe iliyokuwa imeshaka kata kuelekea mikononi mwa askari waliokuwapo mbele kidogo tu hapo kama si kushituliwa na waungwana hao (kushoto)
 Hebu ona hapa alama inayomzuia dereva huyu ilipowekwa Je ni sahihi?
 Njia hii ndivyo ilivyo kuna Mzunguko na njia inayoonyesha kwenda na kurudi na kama picha inavyoonesha ilipowekwa alama kwa jicho lako msomaji je unahisi alama hii imamhusu dereva anayeelekea wapi katika eneo hili au inamzuia kuingia ndani ya jengo hilo haapo mbele?
 Dereva huyu alikuwa akijaribu kugeuza gari fasta ili kumkimbia askari huyu bila mafanikio
Weka hapo pembenei

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.