Habari za Punde

NYOSHI CHOKI, MUUMIN, JUMBE NA WEZAO WAAHIDI MAKUBWA MASHABIKI TAMASHA YA MUZIKI LA 'DIMBA CONSERT'Mwanamuziki mkongwe wa muziki wa dansi nchini, Nyoshi El Saadat, akizingumza katika mkutano na waandishi wa habari leo, wakati wa utambulisho wa Tamasha la 'Dimba Music Concert Kivumbi' linalotaraji kufanyika siku ya Jumamosi kwenye Ukumbi wa Travertine Magomeni,jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mratibu wa onnyesho hilo,Mwani Nyangasa.
Mwanamuziki mkongwe wa muziki wa dansi nchini, Muumin Mwinjuma, akizingumza katika mkutano na waandishi wa habari leo, wakati wa utambulisho wa Tamasha la 'Dimba Music Concert Kivumbi' linalotaraji kufanyika siku ya Jumamosi kwenye Ukumbi wa Travertine Magomeni,jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mratibu wa onnyesho hilo,Mwani Nyangasa.
*************************************
MWAMAMUZIKI nguli Nyoshi El Saadat ‘Rais wa vijana’ amesema muziki wa dansi haujafa licha ya kutopewa nafasi kubwa katika vyombo vya habari nchini.
Rais huyo wa zamani wa bendi ya FC Academia ‘Wazee wa Ngwasuma’ ameyasema hayo katika ukumbi wa CCM Mwinjuma Dar es Salaam, wakati wa mkutano na waandishi wa habari kuelekea Tamasha kubwa la muziki wa dansi lijulikanalo kama ‘Dimba Music Concert Kivumbi’ litakalofanyika katika ukumbi wa Travertine Magomeni keshokutwa Jumamosi.
Tamasha hilo litaanza saa 2 usiku ambapo kutakuwa na pambano kati ya bendi ya Msondo Ngoma chini ya Hassan Rehan ‘Bichuka’ dhidi ya timu ya taifa ya Dansi itayoongozwa na Juma Kakere, Hussein Jumbe, Mwinjuma Muumin, Ally Choki na Nyoshi mwenyewe ambao wametunga nyimbo 10 mpya kwa ajili shughuli hiyo.
“Muziki wa dansi haujafa kama watu wanavyodhani, upo utaendelea kuwepo sababu sisi tupo na kulithibitisha hilo Jumamosi tutashusha burudani ya kutosha Travertine,” alisema Nyoshi.
Mwenyekiti wa kamati wa ya maandalizi ya Tamasha hilo Jim Chika amesema kwa miaka 20 sasa gazeti la Dimba limekuwa likisapoti muziki wa Dansi kwa kuandika lakini wameanza kuandaa matamasha kuendelea kuunga mkono ili kuufikisha mbali.
“Tumekuwa tukiandika stori kuhusu muziki wa Dansi kwa miaka 20, sasa tumeanza kuandaa matamasha na Jumamosi tutakuwa ukumbi wa Travertine katika pambano kati ya Msondo Ngoma na timu ya Taifa ya Dansi,” alisema Chika.
Kwa upande wa Muumin amewataka wadau wa muziki wa Dansi kujitokeza kwa wingi kwakua kutakuwa na ‘suprize’ ya nyimbo mpya huku pia akiahidi kupiga nyimbo ya ‘kikombe kimoja’ siku hiyo.
Kiingilio katika Tamasha hilo VIP itakuwa sh 20,000 kawaida sh 10,000.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.