Habari za Punde

ALLY MAYAY TEMBELE MGOMBEA ALIYEPANIA KUREJESHA DIRA YA SOKA TANZANIA

 Mgombea Urais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania TFF, Ally Tembele Mayai, akizungumza na waandishi wa habari katika Hoteli ya Lamada jijini Dar es Salaam, jana wakati akizindua rasmi Kampeni zake kuelekea uchaguzi huo unaotarajia kufanyika jumamosi Agost 12, mjini Dodoma. Kkulia kwake ni wachezaji wa zamani, Zamoyoni Mogella na Laurance Mwalusako.
************************************************
Na Ripota wa Mafoto Blog, Dar
MGOMBEA urais wa Shirikisho la Kandanda Tanzania (TFF), Ali Mayay amesema kuwa ataanzisha dira ya mpira wa miguu ili kuiwezesha nchi kupata maendeleo makubwa katika sekta hiyo.
Mayay amesema hayo alipokuwa anajinadi katika siku yake ya kwanza ya uzinduzi wa kampeni kuelekea uchaguzi mkuu wa TFF utakaofanyika mkoani Dodoma Agosti 12.
Alisema kuwa kwa sasa hakuna dira ya mpira wa miguu na kuwa chanzo cha kuwa na maendeleo duni kulinganisha na nchi kama Zambia ambayo kwa sasa wanafaidi matunda baada ya kuanzisha na kutekeleza dira hiyo.
“Kwa sasa wachezaji wengi wa Zambia wanacheza soka la kulipwa nje ya nchi, timu yao Taifa inafanya vizuri, Tanzania ina wachezaji wengi wenye vipaji, lakini hakuna dira na kusababisha wao pia kukosa dira katika fani yao,” alisema Mayay.
Alisema kuwa akiwa kama mchezaji, ameweza kuona changamoto mbalimbali za mpira wa miguu na kuamua kugombeanafasi iliyo ili kuzitatua.
Mayay pia alisema kuwa lengo lingine ni kujenga taasisi imara kwa kutumia rasilimali zilizopo kwani tatizo si vipaji, bali ni aina gani ya uongozi unaosimamia mpira wa miguu.
Wachezaji mbalimbali waliong’aa katika medani ya soka hapa nchini, wamepigia chapuo mchezaji wa zamani wa timu ya Taifa, Taifa Stars Ali Mayay kuchaguliwa katika nafasi ya urais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF).
Mgombea huyo ambaye ni chaguo la wachezaji wa zamani nchini aliungwa mkoano na mshambuliaji nyota wa zamani wa labu ya Simba,  Zamoyoni Mogella ambaye alisema TFF inahitaji mtu kama Mayay anayejua matatizo ya mpira wa miguu kwani ameucheza huo mpira.
 Mogella ambaye enzi zake alipewa jina la “Golden Boy” na “Morgan” alisema kuwa wanahitaji kuurudisha mpira kwa wenyewe huku wakiwaomba wagombea kumchagua Mayay.
Alisema kuwa ni wakati wa mabadiliko kwa wadau wa soka nchini kwa kumchagua Mayay ambaye anavigezo vyote katika masuala mbalimbali ya soka na uongozi.
Aliongza kuwa Mayay amecheza mpira katika kiwango cha juu mbali ya kupata elimu ya biashara ambayo imemwezesha kuajiliwa katika serikalini.
“Mayay ni dira ya soka Tanzania, amecheza soka kuanzia shuleni, katika hatua ya vilabu mpaka timu ya Taifa, anajua nini cha kufanya ili kuleta maendeleo ya soka nchini,” alisema Mogella.
Mchezaji wa zamani wa Yanga Mohamed “Adolph” Rishad naye alisema kuwa  Mayay ni suluhisho sahihi kwa maendeleo ya soka nchini na si wagombea wengine.
Rishad amesema kuwa wachezaji wa mpira wa miguu wametengwa katika soka na kukosa mwamko katika mchezo ambao wanaupenda.
Amesema kuwa kwa sasa Tanzania ina matokeo mabaya katika soka la kimataifa ni kukosa uongozi wenye mapenzi ya mchezo pamoja na Tanzania kuwa na vipaji vingi vya soka.
Vile vila Mwalusako na Khaleed Abeid nao wamempigia chapuo mchezaji huyo wa zamani kuchaguliwa katika soka uongozi na kuifanya nchi kufarijika kwa matokeo mazuri.
 Waandishi wa habari wakiwa bize kunasa hotuna ya mgombea huyo.
Baadhi ya wageni waalikwa wakiwa katika mkutano huo.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.