Habari za Punde

BAADA YA KUREKEBISHWA SASA SIMBA KUKABIDHIWA NGAO YAO SEPT 6

 Ofisa Habari wa TFF, Alfred Lucas, akionyesha neno lililokuwa limekosewa katika Ngao ya Jamii ambalo limerekebishwa na kutangaza tarehe ya kuwakabidhi upya timu ya Simba.
Ngao ya Jamii ambayo ilitolewa baada ya Simba kuifunga Yanga kwa penalti 5-4 ikawa imekosewa imeletwa nyingine na itakabidhwa kwa Simba Septemba 6 wakati wa mchezo dhidi ya Azam FC.
Aidha Lucas aliendelea kuomba radhi mashabiki na wapenda soka wote na kuahidi makosa hayo kutojirudia.
Kadhalika mechi nyingine zitachezwa Oktoba 11, mwaka huu ni kati ya Mbao na Azam FC; Kagera Sugar na Mwadui; Mbeya City na Ruvu Shooting; Ndanda na Singida United.
Tarehe hiyo pia Oktoba 11, mwaka huu kutakuwa na mchezo kati ya Njombe Mji na Simba; Mtibwa na Tanzania Prisons; Lipuli na Majimaji wakati Stand United na Young Africans watacheza Oktoba 12, mwaka huu.
Novemba 15, 2017 Mbao itacheza na Young Africans; Kagera na Mbeya City; Stand United na Azam; Mwadui na Ruvu Shooting; Singida na Njombe Mji; Lipuli na Tanzania Prisons; Mtibwa Sugar na Majimaji wakati Novemba 16, Ndanda itacheza na Simba.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.