Habari za Punde

BREAKING NEEEEEEWZ!!!! TUNDU LISSU AONDOKA TENA CHINI YA ULINZI WA POLISI MAHAKAMANI LEO

Mwanasheria Mkuu wa CHADEMA na Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu amechukuliwa na Polisi wakati akitokea Mahakamani alipopatiwa taarifa kuwa anahitajika Kituo Kikuu cha Polisi baada ya kumaliza shughuli za Mahakamani hapo.
Tundu Lissu alikuwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kwenye kesi ya uchochezi inayomkabili lakini pia alikuwa Wakili kwenye kesi ya Yericko Nyerere.
Msemaji wa CHADEMA Tumaini Makene amesema kuwa wakati gari la Lissu likiwa getini tayari kutoka eneo la Mahakama baada kumaliza shughuli za Mahakama lilisimamishwa na Polisi ambao baadhi walimfuata na kumwambia yuko chini ya ulinzi na kutakiwa kwenda kuripoti Kituo cha Polisi cha Kati.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.