Habari za Punde

EMANUEL OKWI AITWISHA MZIGO SIMBA

Emmanuel Okwi, akiwa katika moja ya mechi alipokuwa na timu ya Simba kabla ya kutimka na kurejea tena.
**************************************************************
KOCHA mkuu wa Simba, Joseph Omog raia wa Cameroon amewepa mtihani washambuliaji wa kikosi hicho katika msimu ujao kuhakikisha wanaifungia mabao mengi timu hiyo ili wasirudie makosa ya msimu uliopita ambao walizidwa na wapinzani wao Yanga waliotwaa ubingwa kutokana na tofauti ya mabao.
Kocha huyo amewapa jukumu hilo la kufunga mabao mengi washambuliaji wa timu hiyo wakiongozwa na Mganda, Emmanuel Okwi sambamba na John Bocco ambao wamesajiliwa katika dirisha hili la usajili ambalo linatarajiwa kufungwa keshokutwa Jumapili.
Katika msimu uliopita Simba walifunga mabao …. Kwenye msimu mzima wakati wenzao wa Yanga walifunga mabao na kuwafanya kutwaa ubingwa wa ligi kuu kwa tofauti ya mabao ya kufunga na kufungwa.
Akizungumza jana, Omog amesema kuwa washambuliaji hao wanatakiwa kuifungia timu hiyo mabao mengi kwa ajili ya kuwafanya hata watakapolingana na washindani wao basi wao waibuke na ubingwa.
“Msimu uliopita tulikosa ubingwa dakika za mwisho kabisa tena kwa tofauti ya mabao, sasa jambo hilo sitaki litokee kwa msimu huu na ndiyo maana utaona tumesajili washambuliaji wengi ambao watatufungia mabao kwa kadri ninavyotaka.
“Sitaki kuona tunakuja kupoteza ubingwa wowote ule kwa sababu tu ya kupitwa mabao, sasa ninawapa jukumu hilo washambuliaji wao kuhakikisha tunafunga mabao mengi tutakavyoweza, na kwa sassa naendelea kuwafua wawe vile ambavyo mimi nataka,”alisema Omog.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.