Habari za Punde

HABARI KUTOKA TFF LEO, KIDAO WILFRED KAIMU KATIBU MKUU TFF

Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), imepitisha jina la Kidao Wilfred kuwa Kaimu Katibu Mkuu.
Kidao ambaye ni mchezaji wa zamani wa Taifa Stars ambaye pia Mwenyekiti wa Chama cha Makocha Tanzania (TAFCA), ameteuliwa rasmi jana Agosti 22, 2017 na Kamati ya Utendaji ya TFF. Wasifu wa Kidao utawajia punde.

UAMUZI WA KAMATI YA KIKAO CHA KAMATI YA KATIBA, SHERIA NA HADHI ZA WACHEZAJI
Kamati ya Katiba, Sheria na Hadhi za Wachezaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania, iliyokutana kwa siku mbili mfululizo Agosti 20 na 21, 2017, jijini Dar es Salaam, imepitia usajili wa majina ya klabu 40.
Katika idadi hiyo ya timu 40, kamati imepitia klabu 16 za Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara na Klabu 24 za Ligi Daraja la Kwanza (FDL) kwa mujibu wa katiba na kanuni za mashindano yanayosimamiwa na kuendeshwa na TFF.
Kamati ya Katiba, Sheria na Hadhi za Wachezaji ya TFF, inayoongozwa na Wakili Richard Sinamtwa, imegundua na kubaini kuwa mchezaji Pius Busita amesaini mikataba ya klabu mbili tofauti katika msimu mmoja wa 2017/18.
Kamati imebaini kwamba mchezaji huyo aliyechezea Mbao FC ya Mwanza msimu uliopita, amevunja Kanuni ya 66 ya Ligi Kuu ya Vodacom ambayo inaelekeza adhabu ya kufungiwa mwaka mmoja. Mchezaji huyo amefungiwa kucheza mpira wa miguu kwa mwaka mmoja.
Kamati ya Katiba, Sheria na Hadhi za Wachezaji ya  TFF, imebaini upungufu katika uwasilishaji wa majina ya wachezaji wa msimu wa 2017/18 kwa timu zote.
Klabu imeagiza klabu zote kuleta majina matatu ya wachezaji wasiopungua 18 na wasiozidi 30 wa kikosi cha timu ya vijana (U20).
Klabu zote zimeagizwa kuanisha wachezaji wa zamani na wapya na klabu wakakotoka kwa timu zote mbili za wakubwa na vijana.
Kamati imezitaka klabu hizo pia kuzingatia matakwa ya kanuni kwa kila mchezaji ambaye atapewa leseni ya kushiriki Ligi Kuu ya Vodacom na Ligi daraja la Kwanza.
Matakwa hayo ambayo ambayo yamesisitizwa ni kila mchezaji kujaziwa fomu ya utimamu wa mwili ‘Medical Form’ ya TFF.
Pia Klabu zinatakiwa kuwasilisha nakala tatu za mikataba (Contracts) ya kila mchezaji katika Shirikisho la Mpira wa Miguu (TFF), Uthibitisho wa kukatiwa Bima ‘Insurance’, Barua ya Uhamisho ‘Release Letter’ kutoka timu ambayo ametoka.
Kadhalika sharti jingine linahusu wachezaji wa kigeni ambako kila mchezaji hana budi kuwa na Hati ya Uhamisho wa Kimataifa (ITC) na kulipwa Ada ya ushiriki ya msimu Sh. 2,000,000.
Klabu zimeagizwa kikamilisha utaratibu wa usajili kabla ya Agosti 24, 2017.

RAIA KARIA AMTEUA NYAMLANI, MGOYI
.Pia ateua viongozi mbalimbali wa kamati 
Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania, Wallace Karia amewateua Makamu wa Rais wa zamani wa TFF, Athuman Nyamlani na Ahmed Mgoyi kuwa Wajumbe wa Kamati ya Utendaji ya TFF.
Rais Karia ameteua kwa kwa mujibu wa mamlaka aliyonayo katika Katiba ya TFF ikiwa ni wiki moja baada ya kupatikana kwa viongozi wa shirikisho katika uchaguzi mkuu uliofanyika Agosti 12, mwaka huu.
Rais Karia aliwatambulisha viongozi hao kwenye Kikao cha Kamati ya Utendaji iliyofanyika Jumanne Agosti 22, mwaka huu jijini Dar es Salaam.
Katika kikao hicho pia Rais Karia alitumia fursa hiyo kutangaza viongozi wa kamati mbalimbali za TFF zikiwamo za kinidhamu na kisheria.
Kamati ya Nidhamu: Mwenyekiti Tarimba Abbas, Makamu Mwenyekiti, Peter Hella wakati wajumbe ni Boniface Lyamwike, Dk. Bill Haonga na Kassim Dau.
Kamati ya Rufani za Nidhamu: Mwenyekiti ni Wakili Rahim Zuber Shaban; Makamu Mwenyekiti, Stella Mwakingwe wakati Wajumbe ni Abbas Mtemvu, Amani Mulika na Siza Chenja.
Kamati ya Maadili: Mwenyekiti ni Wakili Hamidu Mbwezeleni, Makamu Mwenyekiti ni Wakili Steven Zangira wakati Wajumbe ni Glorious Luoga, Walter Lungu na Amin Bakhressa.
Kamati ya Rufaa ya Maadili: Mwenyekiti ni Wakili Ebenezer Mshana; Makamu Mwenyekiti ni DCP. Mohammed Mpinga na wajumbe  ni Wakili Benjamin Karume, George Mayawa na ASP. Benedict Nyagabona.
Kamati ya Uchaguzi: Mwenyekiti ni Revocatus Kuuli; Makamu Mwenyekiti ni Wakili Mohammed Mchengerwa; Wakili Edwin Mgendera; Wakili Kiomoni Kibamba na Wakili Thadeus Karua.
Kamati ya Rufani ya Uchaguzi: Mwenyekiti ni Kenneth Mwenda; Makamu Mwenyekiti ni Jabir Shekimweri na Wajumbe ni Wakili Rashid Sadalla, Irene Kadushi na Mohammed Gombati.
Kamati ya Katiba, Sheria na Hadhi za Wachezaji: Mwenyekiti ni Elias Mwanjala; Makamu Mwenyekiti ni Wakili Malangwe Mchungahela wakati Wajumbe ni Zakaria Hanspope, Robert Selasela, Goodluck Moshi, Mhandisi Issa Batenga na Hamis Semka.
Kamati ya Fedha na Mipango: Mwenyekiti ni Michael Wambura; Makamu Mwenyekiti ni Francis Ndulane na Wajumbe ni Almas Kasongo, Pascal Kihanga, Maximillian Tabonwa, Paul Bilabaye na Farid Abeid.
Kamati ya Mashindano: Mwenyekiti ni Ahmed Mgoyi; Makamu Mwenyekiti ni James Mhagama wakati Wajumbe ni Kenneth Pesambili, Shafii Dauda, Fortunatus Kalewa na Mhandisi Andrew Makota.
Kamati ya Ufundi: Mwenyekiti ni Vedastus Lufano; Makamu Mwenyekiti ni Issa Bukuku na wajumbe ni Sarah Chao, Ally Mayay, Michael Bundala, Omar Abdulkadir na Israel Mujuni.
Kamati ya Soka la Vijana: Mwenyekiti ni Khalid Abdallah; Makamu Mwenyekiti ni Lameck Nyambaya na Wajumbe ni Mohammed Aden, Ramadhani Nassib, Salim Kibwana na Vicent Majili.
Kamati ya Mpira wa Wanawake: Mwenyekiti ni Amina Karuma; Makamu Mwenyekiti ni Rose Kissiwa na Katibu wa Kamati hiyo ni Somoe Ng’itu wakati Wajumbe ni Zena Chande, Beatrice Mgaya, Sofia Tigalyoma, Zuhura Kapama na Nia Mjengwa.
Kamati ya Waamuzi: Mwenyekiti ni Saloum Chama; Makamu Mwenyekiti Joseph Mapunda wakati Wajumbe ni Nassib Mabrouk, Leslie Liunda na Soud Abdi.
Kamati ya Habari na Masoko: Mwenyekiti ni Dunstan Mkundi; Makamu Mwenyekiti ni Mbasha Matutu wakati Wajumbe ni Imani Kajura, Mgaya Kingoba, Godfrey Dilunga na Samson Mbamba.
Kamati ya Ukaguzi wa Fedha: Mwenyekiti ni Yahya Hamad; Makamu Mwenyekiti ni Athuman Nyamlani na Wajumbe ni Khalifa Mgonja, Japhary Kachenje, Jackson Songoro na Benesta Rugora.
Kamati ya Tiba: Mwenyekiti ni Dkt. Paulo Marealle; Makamu Mwenyekiti ni Dkt. Fred Limbanga Wakati wajumbe ni Dkt. Norman Sabun, Dkt. Lisobina Kisongo, Dkt. Eliezer Ndalama, Dkt. Elson Maeja na Violet Lupondo.
Kamati ya Futsal na Beach Soccer: Mwenyekiti ni Ahmed Mgoyi; Makamu Mwenyekiti ni Hussein Mwamba na Wajumbe ni Blassy Kiondo, Isaac Munisi, Didas Zimbihile na Aaron Nyanda.
Kamati ya Ajira: Mwenyekiti ni Issa Bukuku; Makamu Mwenyekiti ni Saloum Chama wakati Wajumbe ni Athuman Kihamia, Mtemi Ramadhani, Noel Kazimoto na Hawa Mniga.
Kamati ya Leseni za Klabu: Mwenyekiti ni Wakili Lloyd Nchunga; Makamu Mwenyekiti Wakili Emmanuel Matondo wakati Wajumbe ni Profesa Mshindo Msolla, Hamisi Kissiwa na David Kivembele.
Kamati ya Rufaa za Leseni: Mwenyekiti Wakili Dk. Damas Ndumbaro; Makamu Mwenyekiti ni Wakili Alex Mngongolwa Wajumbe ni Meneja wa zamani wa Uwanja wa Taifa, Charles Matoke, Tumainiel Mlango na Ahmed Menye.

TIMU SITA KUPANDA LIGI KUU MSIMU WA 2018/19 
Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) litapandisha idadi ya timu zinazoshiriki Ligi Kuu msimu ujao wa 2018/19 kutoka 16 za sasa hadi 20, imefahamika.
Uamuzi huo umefanyika Jumanne Agosti 22, 2017 wakati Kamati ya Utendaji inafanya marekebisho ya Kanuni za Ligi Daraja la Kwanza inayotarajiwa kuanza Septemba 16, mwaka huu.
Kwa marekebisho hayo, timu zitakazoshuka daraja msimu ujao kutoka Ligi Kuu ya Vodacom ya sasa ni mbili hivyo kubaki 14. Na ili kufikia timu 20, timu sita (6) za Ligi Daraja la Kwanza zitapanda daraja.
Kwa mujibu wa utaratibu wa Ligi Daraja la Kwanza, timu, ina maana kwamba msimu huu timu mbili zitapanda kutoka katika kila kundi katika ligi hiyo ambayo inatarajiwa kuanza Septemba 16, mwaka huu.
Makundi ya Daraja, kundi ‘A’ lina timu za African Lyon, Ashanti United, Friends Rangers za Dar es Salaam, JKT Ruvu na Kiluvya United za Pwani, Mgambo JKT ya Tanga, Mvuvumwa ya Kigoma na Polisi Moro ya Morogoro.
Kundi ‘B’ ziko za Coastal Union ya Tanga; JKT Mlale ya Ruvuma; KMC ya Dar es Salam, Mawezi Market ya Morogoro, Mbeya Kwanza ya Mbeya, Mufundi United ya Iringa, Mshikamano na Polisi Dar za Dar es Salaam.
Kundi ‘C’ lina timu za Alliance School, Pamba na Toto 
African za Mwanza, Rihno Rangers ya  Tabora, Polisi Mara ya Mara, Polisi Dodoma ya Dodoma, Transit Camp ya Shinyanga na JKT Oljoro ya Arusha.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.