Habari za Punde

JULIO 'MZEE WA KURA MBILI' ASHUKURU KUPATA KURA MBILI BILA KUKESHA, BILA KUTOA HELA

KOCHA mwenye maneno mengi wa zamani wa Simba ambaye alikuwa ni mmoja kati ya wagombea wa nafasi ya Ujumbe katika uchaguzi mkuu wa TFF, uliomalizika jana amesema anashuru kwa kupata kura mbili kati ya kura 128 zilizopigwa.
Akizungumza na mtandao huu wa www.sufianimafoto.com, baada ya matokeo ya uchaguzi huo, Julio alisema kuwa alifikishwa kituoni. ashukuru na kufurahi kwa kupata kura mbili kutokana na yeye kutotumia nguvu kibwa katika uchaguzi huo.
Aliendelea kusema kuwa kuna baadhi ya wagombea wenzake anawajua ambao walitumia nguvu kubwa wakikesha na kutoa hela ili washinde lakini wameangukia pua na wengine hawakuoata hata hizo kura 2.
"Kwa upande wangu mimi nashukuru mungu kwa kupata hata hizo angalau kura mbili, bila kukesha wala kutoa hela kama baadhi ya wagombea mimi ndo kwanza niliuchapa usingizi vizuri tu nikisubiri tulutane kilingeni". alisema Julio
Julio akijadiliana jambo na wadau baada ya matokeo ya uchaguzi huo nje ya ukumbi wa St Gaspar
************************************
Katika uchaguzi huo wagombea wa nafasi ya Ujumbe walikuwa 13 ambapo katika Kanda ya Dar es Salaam, waliochuana angalau kwa karibu ni Lameck Nyambaya aliyeibuka na kura 41 na Shafii Dauda kura 21.
Tukio jingine katika uchaguzi huo lilikuwa ni kukamatwa kwa mtu aliyefahamika kuwa ni mtoto wa mmoja kati ya wagombea akiwa chooni na karatasi ya majina ya wajumbe huku pia akiwa na burungutu la hela, ambaye alidakwa na polisi na kufikishwa kituoni.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.