Habari za Punde

KAMATI YA BUNGE YA BAJETI YARIDHISHWA NA UFANYAJI KAZI WA MFUMO WA MALIPO YA KIELETRONIKI

Mkurugenzi wa Kampuni ya Maxcom Africa, Juma Rajabu (kulia) akimwelekeza Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Bajetim Hawa Ghasia, jinsi ya kutumia mashine za Kieletroniki ili kupita katika geti la kuingilia Kituo cha Mabasi yaendayo haraka cha Kivukoni jijini Dar es Salaam, leo mchama jana wakati walipofika kukagua utendaji wa mfumo wa malipo kwa njia ya Kieletroniki. 
*************************************
Na Ripota wa Mafoto Blog, Dar
KAMATI ya Bunge ya Bajeti, imeridhia ufanyaji kazi wa mfumo wa malipo ya kieletroniki wa uliofungwa na kampuni ya Africa Maxcom katika mradi wa mabasi yaendayo haraka(UDART).
Akizungumza jana jijini Dar es Saalam, katika ziara ya kukagua mifumo hiyo katika vituo vya mabasi vya mradi huo, Mwenyekiti wa kamati hiyo, Hawa Ghasia alisema wajumbe hao wa kamati hiyo wameridhishwa na mfumo huo.
Mwenyekiti huyo aliongeza kuwa kamati hiyo imefurahishwa na mafanikio yaliofikiwa na kwamba inatarajia kuishauri zaidi vyombo vingine vinavyohusika katika utekelezaji wa ukusanyaji wa mapato kwenye mradi huo.

Alisisitiza kuwa  kamati hiyo imereidhishwa na utekelezaji wa agizo la serikali la kukusanya mapato kwa kutumia mfumo huo wa kieletroniki na kwamba ni dhahiri imeonesha kuwa ukusanyaji mapato katika mradi huo umeongezeka ikilingwanishwa na awali.
"Kikubwa kinachofanyika ni kuwa kampuni ya Maxcom ni kama makonda katika mradin huu ambapo ndio wanakusanya nauli ya abiria hivyo imefanikiwa kwa kiasi kikubwa,"alisema.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Maxcom, Jameson Kasati alisema kwa sasa mradi huo umeleta mafanikio makubwa ambapo imeongeza idadi kubwa ya abiria.
Alisema ziara hiyo ni muhimu kwa kamati hiyo kufahamu kwa undani utekelezaji wa mfumo huo wa malipo ambapo umesaidia kupunguza usumbufu kwa abiria.

"Mfumo huu umesaidia kuongeza huduma ya usafirishaji abiria kutoka 50,000 hadi 200,000 hivyo ni dhahiri kuwa mfumo huu ni mzuri katika ukusanyaji wa mapato nchini,"alisema.
Pia, alitaja baadhi ya changamoto ya mfumo huo ni ucheleweshaji wa mtandao hivyo kusababisha usumbufu mkubwa kwa wateja.
Alisema huduma ilianza Mei 16, Mwaka jana ambapo ilianza kwa awali abiria walikuwa 30,000 kwa siku ambapo kwa mizei mitatu waliongezeka na kufikia 200,000.
Mkurugenzi huyo alisema kwa sasa mfumo huo unahudumia abiria 250000 kwa siku hivyo inasaidia kurahisisha hutoaji huduma kwa wateja.
Alizitaja baadhi ya changamoto ambazo zinaikumba katika mfumo huo ni kutokuwepo kwa elimu kwa jamii kwani wengi hawafahamu umuhimu wa mfumo huo ambao unasaidia kudhibiti upotevu wa mapato serikalini.
 Maelekezo yakiendelea.....
 Baadhi ya Wajumbe wa Kamati hiyo wakipanchi tiketi zao ili kuingia ndani ya kituo hicho.
 Deo kutoka Maxcom akitoa maelekezo kwa Mwenyekiti Hawa Ghasia
Mkurugenzi Mtendaji wa Maxcom Africa, Jameson Kasati, akizngumza na waandishi wa habari baada ya ziara ya Kamati hiyo.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.