Habari za Punde

KARATE KUPIGWA AGOSTI 18

CHAMA cha Karate Tanzania (TASHOKA), kimetangaza kuwa michuano ya karate ya Taifa itafanyika kupigwa Agosti 18, mwaka huu,.
Michuano hiyo inatarajia kupigwa katika Uwanja wa Ndani wa Taifa, Dar es Salaam kwa ajili ya kusaka wachezaji watakawakilisha Taifa katika michuano ya kuwania kufuzu Olimpi mwaka 2020.
Akizungumza Dar es Salaam, jana, Rais wa TASHOKA, Sensei Rwezaula alisema kuwa michuano hiyo itashirikisha mikoa nane ambayo imefuzu katika mapambano ya mchujo.
Rwezaula, alizitaja timu za Dar es Salaam, Mbeya, Kigoma, Tanga, Mwanza, Morogoro na Arusha kuwa ndio pekee zitakazocheza michuano hiyo ya Taifa ambayo itafanyika kila mwaka.
Alisema michuano hiyo itasaidia kupata wachezaji vijana kwa ajili ya kuwakilisha Taifa katika mashindano ya Olimpiki ambayo yatafanyika mwaka 2020.
Rwezaula alisema kuwa TASHOKA imedhamiria kuipandisha kiwango karate kimataifa kwa kuwa mchezo huo umekuwa na mafanikio makubwa katika nchi za Afrika.
"Mashindano ya karate Taifa yatafanyika Agosti 18 mwaka huu, yatakuwa na malengo ya kutafuta vijana wenye vipaji na uwezo wa kutuwakilisha vyema katika michuano ya Olimpiki 2020," alisema Rwezaula.
Aliwataka wapenzi wa karate kujitokeza kwa wingi kushuhudioa michuano itakapoanza kwa kuwa itaongeza motisha kwa wachezaji hususani vijana kujituma.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.