Habari za Punde

KATIBU MKUU SIHABA NKINGA AWAHIMIZA MAAFISA MAENDELEO YA JAMII KUHAMASHA ARI YA UFANYAJI KAZI KWA WANANCHI

 Katibu Mkuu Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto anayeshughulikia Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii Bibi Sihaba Nkinga akizungumza na  Maafisa Maendeleo ya Jamii na Maafisa Ustawi wa Jamii Mkoani Iringa wakati alipofanya ziara Mkoani hapo kuangalia utekelezaji wa Sera ya Maendeleo ya Jamii.
******************************************************
Na Raymond Mushumbusi WAMJW
Katibu Mkuu Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia wazee na Watoto anayeshughulikia Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii Bibi Sihaba Nkinga amewaasa maafisa Maendeleo ya Jamii na Maafisa Ustawi wa Jamii nchini kuamsha ari ya kufanya kazi kwa wananchi ili kujiletea maendeleo.
Ameyasema hayo wakati alipokutana na kuzungumza na Maafisa Maendeleo ya Jamii na Maafisa Ustawi wa Jamii mkoani Iringa alipokuwa akifanya ziara kujionea utekelezaji wa Sera ya Maendeleo ya jamii nchini.
Bibi Sihaba Nkinga ameongeza kuwa viongozi wa Halmashauri na Mikoa nchini wanatakiwa kuwapa nafasi Maafisa Maendeleo ya Jamii na Maafisa Ustawi wa Jamii ili kurejesha ari ya wananchi kujitolea katika kutekeleza shhughuli za kimaendeleo katika maeneo yao.
“ Nawaomba Maafisa Maendeleo ya Jamii na Maafisa Ustawi wa Jamii mtimize majukumu yenu ipasavyo ili kuamsha ari ya ufanyaji kazi kwa wananchi ili kuleta maendeleo katika maeneo yao” alisema Bibi Sihaba.
Katibu Mkuu Bibi Sihaba Nkinga pia amesisitiza matumizi ya rasilimali zilizopo ili kuendelea kuhimiza wananchi kujitolea katika kujitolea na kufanya kazi zitakazowaletea maendeleo katika maeneo yao.
Aidha kwa upande wake Katibu Tawala wa Mkoa wa Iringa Bibi Waumoja Ayoub  amemuakikishia Katibu Mkuu Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto anayeshughulikia Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii Bibi Sihaba Nkinga kuwapa ushirikiano Maafisa Maendeleo ya Jamii na Maafisa Ustawi wa Jamii ili waweze kutimkiza majukumu yao.
“Sisi viongozi wa mkoa tupo tayari kutoa ushirikiano kwa Maafisa hawa ili kuwawezesha kutimiza majukumu yao kwa wakati na katika ufanisi” alisema Bibi Waumoja.
Katibu Mkuu Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto anayeshughulikia Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii Bibi Sihaba Nkinga amefanya ziara mkoani Iringa kwa lengo la kujionea utekelezaji wa Sera ya Maendeleo ya Jamii na kuamsha aerinya wananchi katika kujitolea kufanya kazi kwa maendeleo yao na taifa kwa ujumla. 
 Katibu Tawala wa Mkoa wa Iringa Bibi Waumoja Ayoub akisistiza jambo kwa  kwa Maafisa Maendeleo ya Jamii na Maafisa Ustawi wa Jamii Mkoani Iringa wakati Katibu Mkuu Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto anayeshughulikia Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii Bibi Sihaba Nkinga alipofanya ziara Mkoani hapo kuangalia utekelezaji wa Sera ya Maendeleo ya Jamii.
 Mkurugenzi wa Maendeleo ya Jamii Bw. Patrick Golwike akifafanua jambo kwa Maafisa Maendeleo ya Jamii na Maafisa Ustawi wa Jamii Mkoani Iringa wakati Katibu Mkuu Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto anayeshughulikia Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii Bibi Sihaba Nkinga alipofanya ziara Mkoani hapo kuangalia utekelezaji wa Sera ya Maendeleo ya Jamii.
Baadhi ya Maafisa Maendeleo ya Jamii na Maafisa Ustawi wa Jamii wa Mkoa wa Iringa wakimsikiliza Katibu Mkuu Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto anayeshughulikia Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii Bibi Sihaba Nkinga(hayupo pichani) wakati Katibu Mkuu huyo alipofanya ziara Mkoani hapo kuangalia utekelezaji wa Sera ya Maendeleo ya Jamii.

Kikundi cha Sanaa cha Malezi na Uhamasishaji wa Ulinzi kwa Mtoto Wilaya ya Iringa wakiimba wimbo wa kumshukuru Katibu Mkuu Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto anayeshughulikia Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii Bibi Sihaba Nkinga kwa kuendelea kuhamasisha Maafisa Maendeleo ya Jamii na ustawi wa JAmii kutekeleza Sera ya Maendeleo ya Jamii. 
Katibu Mkuu Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto anayeshughulikia Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii Bibi Sihaba Nkinga(kulia) akijadiliana jambo na Katibu Tawala wa Mkoa wa Iringa Bibi Waumoja Ayoub  mara baada ya kumalizika kwa kikao kati ya Katibu Mkuu huyo na Maafisa Maendeleo ya jamii na Maafisa Ustawi wa Jamii Mkoani Iringa. Picha na Erasto Ching’oro WAMJW. 

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.