Habari za Punde

KESI YA KINA AVEVA,KABURU YAAHIRISHWA TENA UPELELEZI BADO, WARUDI MAHABUSU

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu imeiharisha Kesi ya utakatishaji fedha inayomkabili Rais wa Klabu ya Simba, Evans Aveva na Makamu wake, Geofrey Nyange maarufu 'Kaburu' hadi August 16 mwaka 2017 kutokana na kutokamilika kwa upelelezi.
Watuhumiwa hao walifikishwa leo mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Godfrey Mwambapa na wakili wa Serikali, Elia Athanas, ambaye amedai upelelezi wa kesi hiyo haujakamilika, hivyo anaomba ipangiwe tarehe nyingine.
Hakimu Mwambapa alikubali maombi ya wakili wa Serikali Athanas na aliahirsha kesi hiyo hadi August 16 mwaka huu.
Aveva na Kaburu wamerudishwa tena mahabusu mpaka kesi yao itakapotajwa tena.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.