Habari za Punde

KESI YA WEMA SEPETU KUJULIKANA AGOSTI 18 MWAKA HUU

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu leo imweka wazi kuwa Agost 18 mwaka huu itatoa uamuzi kama kielelezo cha msokoto mmoja na vipisi viwili vya bangi vipokelewe mahakamani hapo kama kielelezo vya kesi inayomkabiri Wema Sepetu ama la. 
Uamuzi huo unatarajiwa kutolewa na Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba baada ya majibishano makali kuhusu kielelezo kutoka upande wa utetezi na ule wa mashtaka.
Kielelezo hicho cha bangi kinataka kutolewa katika kesi ya kutumia dawa za kulevya inayomkabili Miss Tanzania 2006, Wema Sepetu na wenzake wawili.
Hatua hiyo imekuja baada ya Wakili wa Serikali, Costantine Kakula kumuongoza shahidi wa kwanza wa upande wa mashtaka, Mkemia kutoka ofisi ya Mkemia Mkuu wa Serikali, Elias Mulima kuendelea kutoa ushahidi wake.
Katika ushahidi wake, shahidi huyo amidai kuwa alipima msokoto huo na vipisi hivyo vya bangi vinavyodaiwa kukutwa nyumbani kwa Wema na kugundua ni bangi.
Mbali na mambo mengine, shahidi Mulima kupitia Kakula aliomba kuitoa kielelezo cha bangi kikiwa ndani ya bahasha iliyofungwa ikiwa na muhuri juu, na kama kielelezo cha ushahidi lakini wakili wa utetezi Tundu Lissu alibisha vikali na kusema, upande wa mashtaka ulisema unataka kutoa bangi lakini sasa wanatoa bahasha.
Wakili Lissu alipinga na kusema, ndani ya bahasha hiyo kuna vitu zaidi ya msokoto mmoja na vipisi viwili vinavyodaiwa kuwa ni bangi.
Alidai Lissu vipisi viwili vyenye majani ukiviangalia kwa makini ni vipisi vya sigara za kienyeji ambayo imetumika kwa sababu vina alama ya kuungua ambavyo kwao vinaitwa twagooso.
Baada ya mabishano makali baina ya pande hizo mbili, Hakimu Thomas Simba aliahirisha kesi hiyo hadi Agosti 18, kwa ajili ya uamuzi kama bangi hiyo ipokelewe au la.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.