Habari za Punde

KIBURI CHA LEIPZIG KINAVYOPAMBANA NA PESA ZA LIVERPOOL

Abdula Dunia, Dar
"UKAE juu ya kiti. Ili uandike hati, ndogo ya wasia. Mimi kwako ni baba. Hati hii ya huba. Andika iwe akiba. Asaa itakufaa. Aliwahi kuandika mwalimu wa lugha ya kiswahili hayati Shaaban Robert katika moja ya kitabu chake cha Utenzi wa hati.
Robert ni moja kati ya waandishi mahiri sana katika kutumia lugha ya kiswahili duniani. Kipaji chake katika hilo ndio kimemfanya aonekane nguli kila mahali. Hakika Shaaban Robert ni nguli wa lugha tamu ya kiswahili duniani. Tuachane na hilo.
Klabu ya Liverpool imetahabika katika kupata kiungo mkabaji wa kuimarika kwa kipindi kirefu tangu walipoondoka viungo wake Xabi Alonso na Xavier Masherano ambao walitimkia Real Madrid na FC Barcelona. Hakika Maschesrano na Alonso walikuwa roho ya Liverpool kwa miaka ile.
Unakumbuka kile kilichotokea Instambul mwaka 2005? Hadi tunakwenda mapumziko AC Milan anaongoza kwa mabao 3-0. Kilichotokea katika kipindi cha pili ni kama maajabu yaliyofanywa na Barcelona dhidi ya PSG katika hatua ya mtoano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya (UCL). 
Tuwaacheni mashabiki wa Liverpool waendelee kuipenda timu yao tu. Tuwaacheni haina jinsi. Kwa mpira ule uliopigwa Instanmbul hakuna shabiki anayeweza kuitosa Liverpool. Hakika tuwaacheni tu.
Katika kufanya vubaya kwa Liverpool miaka ya hivi karibuni hususani kutoshiriki katika michuano ya UCL kwenye miaka kadhaa imetokana na kukosa kikosi imara ikiwemo kiungo mkabaji. 
Tukiachana na Jordan Henderson ambaye ni mzuri zaidi katika nafasi ya kungo mlishaji yaani namba nane kulikuwa na Lucas Leiva ambaye ni mkabaji mzuri ila sio mzuri kuiopoozesha timu pamoja na kuanza mashambulizi. Sio kiongozi wa viungo wenzake. Hiyo ndio ilikuwa sababu ya Liverpool kufanya vibaya katika miaka ya hivi karibuni.
Liverpool ilikosa kiungo kiongozi. Gerard alikuwa kiongozi. Alonso na Maschesrano pia walikuwa viongozi. Kwa nini Liverpool ya sasa inakosa kiungo kiongozi kwa ajili ya kuwamiliki wenzake pale dimbani? 
Hakuna timu inayotwaa ubingwa wa Ligi Kuu au UCL Ulaya bila ya kuwa na kiungozi kwa wenzake. Kulikuwa na Patrick viera, Roy Keane, Yaya Toure, Paul Schooles, Ng'olo Kante na wengineo hao ni wachache tu.
Liverpool inahitaji kiongozi wa kati, inahitaji mshindi wa mipira ya kati yaani Ball Winner, mshindaji wa mipira yote yaani ya chini na juu ya uwanja. Inahitaji kiungo anayefanya kazi kupita kiasi, mtu wa kucheza mipira ya pasi za haraka baada ya kukaba.
Katika moja ya maandiko ya Hayden Ferry, mchezaji wa mpira wa miguu nchini Marekani aliwahi kusema kuwa mpira ni sawa na maisha. 
"Hakika soka ni sawa na maisha, lazima ujifunze kucheza kutokana na kanuni zake zinavyosema," Hakika Liverpool inahitaji kiungo mahiri atakayecheza kutokana na kanuni zote za mkabaji.
Siku za hivi karibuni katika kulijua hilo, kocha wa Liverpool Jurgen Klopp ameamua kutumia nguvu zake kubwa kuishawishi timu yake kumsajili kiungo wa RB Leipzig, Naby Keita. Hakika Klopp hajawahi kubahatisha katika kiungo mkabaji wa uhakika.
Tuliwahi kushuhudia kwa Sven Bender na Jakub Blaszczykowski. Hakika watu hawa hawakuwa na masihara kabisa. Mnaikumbuka ile Borussia Dortmund iliyoifunga 4-0 Real Madrid? Madrid anakula hizo anatolewa kwa tofauti ya mabao katika Ligi ya Mabingwa. Kilio cha Dortmund katika fainali baada ya kufungwa na Bayern munich kilikuwa sahihi kabisa.
Acha Klopp aendelee kupambana na Keita. Acha Keita aendelee kuwa na ndoto za kucheza Livepool. Keita anapenda kucheza Liverpool anahitaji kuwa pale hata leo hii. Kiburi cha Mwenyekiti wa Leipzig, Oliver Mitzlaff kinaendelea kumuumiza Keita. Kocha wa Leipzig, Ralph Hasenhüttlalishakubali mapema kuwa moyo wa Keita ni wa Liverpool lakini Mitzlaff anaendelea kumletea kiburi yule mwenyekiti makini wa Liverpool, Tom Werner.
Kugomea mazoezi, kumchezea rafu mbaya mchezaji mwenza katika mazoezio ni baadhi ya matokeo yanayoonyesha kuwa Keita anahitaji kuwa wa Liverpool sio wa Leipzig tena. Matukio ya Keita yanaonyesha kuwa moyo wake upo kwa Klopp na mwili wake pekee ndio wa 
Liverpool inahitaji mkabaji wa moja kwa moja. Keita ni suluhisho yaani ni mkabaji wa uhakika 'box to box'. Ana uwezo wa kufunga ni kiongozi wa wenzake na anapiga pasi za uhakika. Hakika Keita ni dawa ya Klopp pale Liverpool.
Naweza kusema kuwa hadi sasa Liver haina ‘Box to Box midfielder’ anayeweza kucheza kama Keita. Klopp anataka saini ya Keita kwa sababu anahitaji ulinzi mkubwa kwa mabeki na wakati huo huo anahitaji washambuliaji wake wapumzike.
Anahitaji Sadio Mane, Phillipe Coutinho, Mohamed Salah na Firmino wawe huru zaidi na wasiwe na mzigo mkubwa wa kukaba. Keita huenda akaongeza nguvu ya Liverpool kupigania taji la EPL kwa nguvu zote kwani vijogoo watahitaji kikosi kipana ili kuanza mapambano kwa kujiamini.
Keita ataisaidi Liverpool. Klopp hajawahi kubahatisha katika kumsajili mchezaji mkabaji. Keita anakila sababu za kuwa chaguo la Klopp. Kuwa na kiungo kama Keita kwa sasa ni muhimu kwa timu yoyote. Keita hana utofauti na Granit Xhaka, Ngolo Kante na Carlos Casemiro. Hakika hawa ndio viungo wanaotakiwa kwa sasa.
Keita ana zile kazi saba za kiungo yoyote mkabaji bora ambazo lazima awe nazo. Keita anakaba kwanza, analinda mabeki wake, ni mzuri katika mipira ya kulala kuhakikisha anazuia hatari langoni kwake.
Keita anauwezo wa kuwamiliki viungo wa timu pinzani, ni mzuri katika kupiga pasi za haraka baada ya kukaba. Keita ni kiongozi kwa wenmzake, Hakika anakila sababu za kuisaidia Liverpool. Tuendelee kuona filamu hii ya Keita na kiburi cha mwenyekiti wa Leipzig inavyoendelea kushika hatamu.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.