Habari za Punde

LIVE: MATUKIO YA AWALI YANAYOENDELEA UWANJA WA TAIFA MUDA HUU KABLA YA MTANANGE WA YANGA VS SIMBA

 Shabiki wa Simba ambaye pia aliibuka kidedea na kutwaa zawadi ya shabiki bora wa Ndondo Cup, akiongoza mashabiki wa Simba kuingia katika viwanja vya Uwanja wa Taifa kwa ngoma ya Mdundiko kuelekea mchezo wa Ngao ya Jamii unaotarajia kuanza majira ya saa kumi na moja uwanjani hapa
 Mashabiki wa Simba wakiingia kwa shangwe maeoeneo ya Uwanja wa Taifa.
 Shabiki wa Yanga aliyevaa jezi iliyoandikwa jina la kiungo Ajibu akikatika mitaa ya Uwanjani hapo kuelekea kuingia uwanjani.
 Mashabiki wa Simba wakisebeneka
 Mashabiki wa Yanga wakiwa katika foleni kuingia uwanjani hapo
 Mashabiki wa Yanga wakiwa katika foleni wakichanganyikana na mashabiki wa Simba katika geti la upande wa Yanga jambo ambalo ni nadra kutokea na hasa wakati zinapocheza timu hizi.
 Mashabiki wa Simba wakiwa katika foleni ya kuingia getini Uwanja wa Taifa lakini huku hakuna shabiki hata mmoja mwenye rangi ya njano kama ilivyo geti la upande wa Yanga, hii inaashiria nini????
Mashabiki wa Simba wakiwa wamebeba Jeneza lililofunikwa kwa bendera ya Yanga.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.