Habari za Punde

MADEGA APANIA KUIREJESHA ZANZIBAR CAF, ATAMBA NA UADILIFU KATIKA UONGOZI

 Mgombea Urais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania TFF, Imani Madega, akizungumza na waandishi wa habari katika Hoteli ya New Africa jijini Dar es Salaam leo mchana wakati akizindua rasmi Kampeni zake kuelekea uchaguzi huo unaotarajia kufanyika jumamosi Agost 12, mjini Dodoma. Kkulia kwake ni wachezaji wa zamani, Zamoyoni Mogella na Laurance Mwalusako. Katikati ni Evarist Hagila.
 MWENYEKITI wa zamani wa klabu ya Yanga na chama cha soka cha mkoa wa Pwani (Corefa), Imani Madega amewaomba wapiga kura kumchagua katika nafasi ya Urais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) kutokana na uadilifu na uzoefu katika uongozi.
Madega amesema hayo wakati wa uzinduzi wa kampeni  huku akijinasibu kuwa taaluma yake ya sheria ni ‘silaha’ tosha ya kuliwezesha shirikisho hilo kuwa na nguvu na kuepuka kuingia mikataba isiyokuwa na tija.
Alisema kuwa nafasi ya kuwa kuongoza TFF inahitaji mtu mwenye muda kwa mujibu wa taratibu za Fifa na Caf na kuwaomba wagombea kuachana na wagombea wenye ajira kwani watakosa muda wa kulitumikia shirikisho hilo.
Alifafanua kuwa cheo cha Urais wa TFF si cha mchezo kwani kinahitaji mtu wa kufanya kazi masaa 24 ili kuwatendea haki wapiga kura, wanachama na wadau wa mchezo wa soka nchini.
“Mimi ni mwanasheria wa kujitegemea, sipangiwi kazi, ni rahisi kulitumikia shirikisho kuliko wagombea wengine, rais wa TFF ndiye mtendaji mkuu, hivyo anatakiwa kupatikana muda wote, anatakiwa kuwa mkazi wa eneo ambalo ofisi kuu inapatikana,” alisema Madega.
Alisema kuwa akiwa  kiongozi wa Yanga, alidhihirisha uadilifu wake kwa kuiachia klabu hiyo fedha taslimu Sh milioni 209 na kuweka historia katika uongozi wa soka nchini.
Kwa mujibu wa Madega, TFF inakabiliwa na chagamoto nyingi ikiwa pamoja na kutothamini mchango wa wanachama wake  wakati wa uendeshaji wa shughuli mbalilmbali na thamani upatiakana wakati wa uchaguzi mkuu tu.
“Mimi nitaondoa mgawanyiko huo na kulifanya shirikisho lenye ushirikiano kati ya TFF na mikoa na vile vile vyama vya wilaya, lengo ni kuhakikisha kuwa na taasisi imara na vijana kupata nafasi ya kucheza mpira katika mazingira mazuri na hivyo kupata wachezaji nyota katika timu ya Taifa,”
“Lengo langu ni kujenga TFF yenye uwezo mkubwa wa kifedha na kusaidia vyama vya mikoa ili kuleta  maendeleo ya soka,  kwa sasa kuna nafasi kubwa kutokana na serikali kuleta sera ya maendeleo ya viwanda ambavyo vitawekeza hapa nchini,” alisema.
Alisema kuwa Tanzania ni nchi yenye rasimali nyingi na wapo wawekezaji wengi wenye nia ya kuwekeza nchini, lakini wanashindwa kutokana na kukosa viongozi waliokosa uaminifu.
Madega pia alisema kuwa atahakikisha mahusiano baina ya TFF na serikali yanakuwa makubwa ili kuendesha gurudumu la maendeleo mpira wa miguu na vile vile kuwekeza katika idara ya ufundi ikiwa makocha na waamuzi.
Kiongozi huyo wa zamani aliongeza kuwa ataboresha soka la vijana na wanawake ili kuleta tija kwa wachezaji chipukizi na wanawake kwa ujumla.
Madega alisema hayo wakati wa mkutano wake wa kwanza wa kampeni uliofanyika jijini jana. Alisema kuwa mbali ya kuwa na sifa mbalimbali, amegundua kuwa kuna watu wanataka kuaharibu
‘Kazi moja, mtu mmoja”, soka siyo jalala la mtu kwenda kupotezea muda
-sijaajiliwa, ni mwanasheria—wakili wa kujitegemea… ni full-time,
‘wagombea wengine wanao huo muda?
Suala la muda wa Rais wa TFF lazima awe na muda kwani ndiye msimamizi mkuu wa shughuli za kila siku za shirikisho,
“lazima awe executive president, lazima awe anaishi mahali ambayo shirikisho lipo,
+ rais wa fifa anatakiwa kuishi zurich, caf cairo ili kuitendea haki kazi anayoifanya-
-         Nyingine ni taaluma yake ya sheria ambayo ni nguzo pekee ya kuwalinda wanachama wako. Taaluma ndiyo itakayomfanya awe mtetezi wa shirikisho,
-         sema kuwa uadilifu
-         viongozi wengi wanapindisha taratibu, taaluma, msimamo 
2010, maliza bila kashfa- niliacha hela milioni 209
 1999- yanga mkurugenzi wa fedha
2004- mwenyekiti wa mkoa wa Pwani (Corefa) na kuasisi uwanja wa soka wa mkoa wa Pwani wa Mabatini, Mlandizi
Timu ya Ruvu Shooting
Pwani Stars na Mzizima- Mwinyi Kazimoto-
TFF- mjumbe wa kamati ya utendaji- kutoka FAT kwenda TFF chini ya Rais Leodegar Tenga
-Marekebisho ya Katiba ya TFF
Yanga—2005 mwenyekiti wa klabu ya Yanga
Rekodi ambazo hazivunjwa
Uadilifu na uaminifu ni chombo muhimu sana katika soka. Mpira unaendeshwa kwa sponsorship,
Wadhamini wengi wanataka kiongozi mwaminifu
-uongozi wa Yanga nilipata misukosuk mingi kwa kushrikiana na taarufa  ya sheria.
Uwekaji wa sekretarieti- Louis Sendeu (TBC) na kuajiliwa na Yanga
Yanga kuifanya kujitegemea- weka mipango thabiti ya kutimiza hilo. Kusajili logo kisheria kwa Yanga na kuilinda. 
Na Abdul Dunia, Mafoto Blog
Madega amesema kuwa atapambana kuirejeshea uanachama Shirikisho la Soka Zanzibar (ZDFA).
Hivi Karibuni Shirikisho la Soka Afrika (CAF) liliifutia hatio ya uanachama ZFA kwa mantiki ya kuwa ndani ya Tanzania hivyo haikukizi vigezo vya kuwa na uanachama.
Madega alitoa kauli hiyo, Dar es Salaam jana, alipokuwa akinadi sera zake katika mkutano wa kampeni kwa waandishi wa habari.
Alisema hatokurupuka katika kuirejesha Zanzibar katika CAF hivyo atahakikisha anapitia hoja za CAF na ufafanuzi kutoka Baraza la Michezo la Taifa kwa ajili ya kujenga hoja ili irudishwe.
Alisema Zanzibar ina kila sababu ya kuwa mwanachama wa CAF hivyo atapambana kuirejesha katika shirikisho hilo na baadae kupata uanachama wa kudumu katika Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA).
Mbali na hilo, Madega alisema kuwa endapo atapata fursa ya kuchaguliwa na kuwa rais atahakikisha anaipeleka timu ya Taifa ya Tanzania 'Taifa Stars' katika viwango vya juu vya FIFA ili wachezaji wake kucheza katika timu mbalimbali duniani.
"Nitahakikisha naibua vipaji vya vijana kwa ajili ya kupata timu bora ya Taifa, nitapambana timu ya Taifa kupata viwango bora vya FIFA ikiwemo kucheza Kombe la Dunia," alisema Madega.
Alisema kuwa atahakikisha anaweka utawala bora katika mikoa na wilaya kwa ajili ya kuibua na kuwakuza vijana wenye vipaji vya kucheza soka ili kupata timu bora ya Taifa.
Madega aliwahi kuwa Mwenyekiti wa Klabu ya Yanga mwaka 2006 hadi 2010 ambapo aliiongoza timu hiyo kwa mafanikio makubwa ikiwemo kuwa na fedha za kutosha ambazo aliiachia klabu hiyo baada ya kumaliza muda wake.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.