Habari za Punde

MAENDELEO YEYOTE YANAPATIKANA KWA WANANCHI KUJITOA

Mbunge wa Mkuranga, Abdallah Ulega akikabidhi sehemu ya mifuko 10 ya Saruji katika kivuko cha karavati ili kuweza kujenga kingo katika kivuko hicho.
*******************************

Na Ripota wa Blog, Mkuranga.
Mbunge wa Mkuranga, Abdallah Ulega amesema kuwa maendeleo yoyote yanapatikana kwa wananchi kujitoa kwa fedha pamoja na nguvu. 
Ulega aliyasema hayo jana katika kijiji cha Chanungu wakati alipopeleka mifuko kumi kwa ajili kusaidia miundombinu ya barabara ya kijiji hicho ambao wamejitoa kufanya upanuzi kwa kungoa mimea yao. 
Amesema kuwa kama viongozi kazi yake ni kusukuma maendeleo pamoja na kuangalia sehemu ambayo inatatizo na kuweka nguvu. 
Ulega amesema kuwa kijiji hicho kiweke mkakati wa kuwa na ukusanyaji mapato yanayotokana na mauzo ya ardhi na fedha hiyo kuweza kutumika katika maendeleo . 
Aidha amesema kuwa maendeleo ya kuwa na Shule na Zahanati katika kijiji hicho kuanza mchakato wa kutafuta maeneo.
Mbunge wa Mkuranga, Abdallah Ulega akizungumza na wananchi wa Chanungu juu ya maendeleo ya kijiji hicho.
.Mwenyekiti wa Chadema katika kijiji jirani cha Chanungu akimpongeza Mbunge, Abdallah Ulega kwa kazi anayoifanya Mbunge wa jimbo hilo. Picha na Emanuel Masaka, Globu ya Jamii.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.