Habari za Punde

WAZIRI MWAKYEMBE KUZINDUA MASHINDANO YA MAGARI YATAKAYOTIMUA VUMBI AGOSTI 5


WAZIRI wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk. Harrison Mwakyembe, anatarajiwa kufungua mashindano ya mbio za magari ya ARC.
Mashindano hayo yatakayofanyika Bagamoyo, Pwani yataanza Agosti 5, mwaka huu kwa kushirikisha waendesha magari kutoka nchi 10.
Akizungumza Dar es Salaam jana, Mratibu wa mashindano hayo, Nizar Jivan alisema mashindano hayo ya 16 Barani Afrika yatashirikisha madereva 15 na kusema maandalizi yapo kwenye hatua za mwisho.
Jivan alisema michuano hiyo itazinduliwa Ijumaa katika Hoteli ya Southern Sun iliyopo jijini Dar es Salaam.
Alisema washindi watatu wa juu watapata nafasi ya kushiriki michuano ya ubingwa wa dunia itakayofanyika nchini India.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.