Habari za Punde

MAKAMU WA RAIS SAMIA SULUHU HASSAN AKUTANA NA BALOZI WA UHOLANZI NCHINI

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan leo amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Uholanzi nchini Mhe. Jaap Frederiks ambaye alifika Ikulu kwa lengo la kuaga baada ya kumaliza muda wake wa kazi hapa nchini.
***************************************
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan leo amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Uholanzi nchini Mhe. Jaap Frederiks ambaye alifika Ikulu kwa lengo la kuaga baada ya kumaliza muda wake wa kazi hapa nchini.
Makamu wa Rais alimhakikishia Balozi huyo kuwa Tanzania itazidi kuimarisha uhusiano wake na nchi ya Uholanzi hasa katika sekta ya kilimo, elimu na uboreshwaji wa mazingira ya uwekezaji ili kufikia lengo la Tanzania ya Viwanda.
Aidha, Mhe.Balozi aliahidi kuwa mjumbe mzuri wa Tanzania na atarejea mara kwa mara kuja kutembea kwani Tanzania ina watu wema na vivutio vingi vya utalii.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa katika picha ya pamoja na Balozi wa Uholanzi nchini Mhe. Jaap Frederiks ambaye alifika Ikulu kwa lengo la kuaga baada ya kumaliza muda wake wa kazi hapa nchini.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza jambo na Balozi wa Uholanzi nchini Mhe. Jaap Frederiks ambaye alifika Ikulu kwa lengo la kuaga baada ya kumaliza muda wake wa kazi hapa nchini.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.