Habari za Punde

MASHINDANO YA TANO YA GOFU KANDA YA AFRIKA MASHARIKI YAANZA KUTIMUA VUMBI LEO GYMKHANA DAR

 MCHEZAJI wa Timu ya Gofu ya Tanzania, Amani Said, akipiga mpira katika Shimo Namba 9, wakati akichuana na mpinzani wake John Karichu, kutoka nchini Kenya, katika mashindano ya Tano ya Kanda ya Afrika Mashariki yanayoshirikisha Nchi Sita za Tanzania, Ethiopia, Kenya, Uganda, Burundi na Rwanda, yaliyoanza jana katika Viwanja vya Gymkhana jijini Dar es Salaam.
 John Karichu, akipiga mpira....
**********************************************
Na Muhidin Sufiani (MAFOTO), Dar
JUMLA ya nchi Sita leo zimeanza mchuano mkali katika mashindano ya gofu ya kanda ya tano ya Afrika yaliaonza kutimua vumbi katika Viwanja vya Gymkhana, jijini Dar es Salaam.
Mashindano hayo ya siku tatu yaliyoanza jana yanazishirikisha nchi za Rwanda,Burundi,Ethiopia,Uganda, Kenya na wenyeji Tanzania.

Katika mchezo uliochezwa jana upande wa ‘Singel’s kati ya Amani  saidi kutoka Tanzania na John Karicho kutoka Kenya wachezaji hao walitoka sare  katika mashimo 18 waliyocheza.

Akizungumza na Gazeti hili baada ya mchuano huo kumalizika, Karicho kutoka Kenya, alisema kuwa mchuano ulikuwa mzuri na wenye upinzani mkubwa kutokana jinsi alivyokuwa nyuma kwa viwanja 3-0 kati ya viwanja 9 walivyocheza.
Aidha Karicho, alisema kuwa uchezaji wa mpinzani wake, Saidi  ni mzuri sana na katika mchezo huo alidai  alicheza kwa uangalifu mkubwa katika viwanja 9 vya mwisho kuhakikisha anasawazisha matokeo hayo.
Kwa upande wake Said, alisema kuwa angeweza kurudi na ushindi kama angecheza vizuri katika viwanja 9 vya mwisho.
“Nimeshangaa sana kwa matokeo haya na sikutegemea kabisa kama mpinzani wangu angeweza kutoa sare na mimi kwa jinsi nilivyokuwa nimembana,”alisema Saidi
Hata hivyo licha ya Amani Saidi kutoka sare katika mchezo wake naye Naodha wa Tanzania  Victor Joseph aliweza kumshinda  kirahisi Baguma Richard kutoka Uganda kwa viwanja 8-7.
Akizungumza baada ya mchezo huo kumalizika Joseph alisema kuwa, hakupata upinzani katika mchezo wake katika viwanja hivyo walivyocheza.

“Niliingia uwanjani kwa kutomdharau mpinzani wangu nilicheza kwa madhumuni ya kuhakikisha namshinda mapema mpinzani wangu,”alisema Joseph.

Hata  hivyo Joseph alisema kuwa anayaona mashindano hayo ya mwaka huu kama yatakuwa magumu zaidi kulinganisha na mashindano ya mwaka jana yaliyofanyika Ethiopia.
Akizungumzia wachezaji  wa nje, Joseph alisema kuwa kiuchezaji wanazihofia zaidi nchi za Kenya na Uganda na kudai kuwa wamekuwa wakiwasumbua  katika mashindano mengi ya kimataifa yaliyopita.
Katika mchezo mwingine  Abdul Dyabar, kutoka Uganda alimshinda Glslassie Ephrem, kutoka Ethiopia kwa 7-0.
Watanzania wengine waliotarajia kucheza jana jioni ni Seif Mcharo na  N. Emanuel kutoka Rwanda,Prosper Herman na Salumu Hakizimana wa Burundi,Richard Mteve na  Abdul Bizimana Burundi, ambapo mchezo wa mwisho utakuwa kati ya Pravir Singh Ghattora na Krova Nahimana wa Burundi.
 Sehemu ya mashabiki wa mchezo huo waliofika kushuhudia mchuano huo

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.