Habari za Punde

MATOKEO YA UCHAGUZI KENYA UPINZANI BADO WALALAMA

Muungano wa upinzani umesema hauungi mkono tangazo linalotolewa na  Tume ya Taifa ya Uchaguzi nchini Kenya.
Msemaji mkuu wa muungano huo, Musalia Mudavadi, amesema malalamiko yaliyowasilishwa na muungano huo kwa tume hayajashughulikiwa mpaka sasa ipasavyo.
Aidha Mudavadi amesema baada ya kukutana na tume hiyo, walifahamishwa kwamba baadhi ya mambo yao yatashughulikiwa baada ya matokeo kutangazwa.
"Mikutano ilikuwa kama shughuli ya uhusiano mwema tu," amesema.
Tume ilikuwa imewaalika maajenti wakuu kwa mkutano kabla ya kutoa tangazo saa moja unusu.
Lakini upinzani umesema hautashiriki katika kukubaliana na tangazo la tume hiyo.
Naibu ajenti wa muungano huo James Orengo ametilia shaka waangilizi ambao walikuwa wamesema uchaguzi ulikuwa huru na wa haki.
Amesema waangalizi hao walifaa kuchunguzwa kwanza.
Bw Orengo amesema pia kwamba muungano huo haupangi kwenda kortini kupinga matokeo.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.