Habari za Punde

MCHENGA BBALL STARS YAANZA VYEMBA YAIBANJUA TMT FAINALI ZA SPRITE


Timu ya mpira wa kikapu ya Mchenga Bball Stars imeanza vyema katika mchezo wa kwanza wa fainali ya Sprite BBall kings kwa kuweza kuibuka na ushindi wa alama 101 dhidi ya 71 vya TMT.
Mchezo huo uliopigwa katika Uwanja wa Don Bosco Oysterbay ulikuwa wa kasi kwa kila upande kwa timu ya TMT Kuonekana kuwabana na kuwalinda Mchenga Bball stars.
Katika mchezo huo wa kwanza wa fainali ya michuano ya Sprite BBall Kings,Mchenga wameweza kuibuka na ushindi wa alama 101 ambapo katika robo ya kwanza na ya pili walionekana kupewa ulinzi mkali na timu ya TMT lakini utulivu, umakini na nidhamu ya wachezaji wa Mchenga uliweza kubadili matokeo katika robo ya tatu na ya nne.
Nahodha wa timu ya TMT  Isihaka Masoud amesema kuwa wamepoteza mchezo wao wa kwanza wa fainali ila bado kuna mechi zingine zinazoweza kuamua matokeo na zaidi wanaenda kuangalia wapi wamekosea ili katika mchezo wa pili wa fainali waweze kuibuka kushinda.
"Tunaenda kuangalia wapi tumekosea, turekebishe na katika mchezo wa pili wa fainali tunataka kuhakikisha tunatoka na ushindi kwani mecho moja haiwezi kuamua matokeo ya mechi zilizobaki," amesema Isihaka.
Fainali hiyo inayoendelea katika viwanja vya Don Bosco iliweza kuhudhuriwa na wasanii mbalimbali kwa ajili ya kushuhudia mtanange huo pamoja na kutoa Burdani kwa mashabiki wa mpira wa kikapu waliojitokeza kushabikia  timu hizi mbili za Mchenga BBall Stars na  TMT zote zikitokea Upanga.
Baadhi ya wasanii waliohudhuria ni pamoja na Young D, Lulu diva, Tammy the baddest, Country Boy ,Kajala, DJ choka na wengine wengi.
Mchezo wa pili wa nusu fainali utapigwa tena Kesho, Jumatano katika Viwanja vya Don Bosco ambapo mshindi wa kwanza atajinyakulia kiasi cha milion 10, mshindi wa pili milioni 3 na mchezaji bora wa michuano (MVP) atajinyakulia milioni 2.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.