Habari za Punde

MCHUNGAJI DKT. ENOCH AMINU KUTOKA GHANA NA MCHUNGAJI INNOCENTIKECHUKWU KUTOKA NIGERIA KUTOA HUDUMA YA UJAZO NA UPAKO TABATA JIJINI DAR

Kanisa jipya la 'Pure Fire miracles Ministries International' lililopo Tabata Segerea Kwa Bibi Barabara ya Lufita, linataja utoa huduma ya Ujazo na uponyaji kwa siku tatu kuanzia jumatatu hadi jumatano.
Katika huduma hiyo atakuwepo Mchungaji Dkt. Enoch Aminu kutoka nchini Ghana na atakayepokelewa na mwenyeji wake Mchungaji Innocent Ikechukwu kutoka Nigeria.
Huduma hiyo itatolewa kwa lengo la kusaidia wanachi wenye matatizo mbalimbali, ili kupata upanyaji na kumtumaini mungu,  ambapo mwendeshaji mkuu wa huduma hiyo, atakuwa ni Dkt. Enoch Aminu kutoka nchini Ghana, inayotarajia kuanza saa 11:00 jioni, baada ya kumpokea Dkt. Enoch Aminu kutoka nchini Ghana, atakayewasili siku hiyo.
Aidha baada ya kuwasili Dkt. Enoch Aminu kutoka nchini Ghana, anatarajia kukutana na waandishi wa habari, kwa ajili ya kuufahamisha umma kusudio la- huduma hiyo.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.