Habari za Punde

MCHUNGAJI DKT ENOCK AMINU WA GHANA ATUA NCHINI KUTOA HUDUMA KWA SIKU TATU KATIKA KANISA LA PURE FIRE MIRACLES, AMFAGILIA RAIS MAGUFULI


Mwanzilishi wa Kanisa la Pure Fire miracles Ministries International, lililopo Tabata Sergerea kwa Bibi, Mchungaji Mkuu Dkt. Enock Aminu, kutoka nchini Ghana, akizungumza na baadhi ya Waumini wa Kanisa hilo baada ya kuwasili nchini juzi kwa ajili ya Ibada maalumu ya siku tatu za huduma ya ujazo na upako, iliyoanza jana jijini Dar es Salaam. 
Mwanzilishi wa Kanisa la Pure Fire miracles Ministries International, lililopo Tabata Sergerea kwa Bibi, Mchungaji Mkuu Dkt. Enock Aminu, kutoka nchini Ghana, akiagana na baadhi ya Waumini wa Kanisa hilo baada ya kuwasili nchini juzi na kuzindua Kanisa hilo kwa ajili ya Ibada maalumu ya siku tatu za huduma ya ujazo na upako, iliyoanza jana jijini Dar es Salaam. Picha na Muhidin Sufiani (MAFOTO)
********************************

Na Ripota wa Mafoto Blog, Dar
KANISA jipya la ‘Pure Fire Miracles Ministries International’, limesema linafurahishwa na utendaji kazi wa Rais, Dk. John Magufuli na kuwataka waumini wake na watanzania kwa ujumla kumuunga mkono kwa kufanya kazi kwa bidii ili nchi iweze kupiga hatua zaidi za maendeleo kupitia uchumi wa viwanda.
Mwanzilishi na Mchungaji Mkuu wa Kanisa hilo kutoka Ghana, Dk. Enoch Aminu aliyasema hayo katika kongamano la huduma ya ujazo na upako linalofanyika kwa siku tatu jijini Dar es Salaam na kuwashirikisha waumini wa dini mbalimbali.
“Namshukuru sana Mungu kwa ajili ya Rais Magufuli kwa kuwa ni mchapa kazi mzuri na amekuwa akifanya kazi zake kwa kumuamini Mungu na kudhihirisha hilo amekuwa akiomba watumishi wamkumbuke katika maombi, hivyo watanzania mnapaswa kuiga na kuunga mkono juhudi zake za kuwaletea maendeleo wananchi wote” alisema.
Alisema kanisa hilo limeanzishwa kwa ajili ya kutoa huduma kwa wote na lengo lao ni kuhubiri amani na upendo ambayo ndiyo msingi wa mafanikio ya Taifa lolote “bila amani hakuna maendeleo na penye ugomvi, vita na chuki hakuna maendeleo, tunaamini ukipanda mbegu ya amani na maendeleo yataonekana”.
Alisema ujumbe katika kongamano hilo ni “Mungu wa Mafanikio’ wakiamini kwamba Tanzania imebarikiwa hivyo ni wakati wa sasa wa kumiliki raslimali zao kama ilivyo katika maandiko.
Mapema Mchungaji kutoka Nigeria, Innocent Ikechukwu alisema katika kongamano hilo wananchi wenye matatizo mbalimbali watasaidiwa kwa kupatiwa huduma ya maombi na kupata uponyaji na kufundishwa jinsi ya kumtumainia Mungu katika kuyafikia mafanikio.

Alisema huduma hiyo inafanyika kwa siku tatu kuanzia saa 11.00 jioni katika eneo la Kanisa hilo lililopo barabara ya Rufia  eneo la Segerea kwa bibi huku huduma za kawaida zikiwa ni kila siku ya jumapili kuanzia saa 1.30 asubuhi hadi saa 4.30 asubuhi na katikati ya juma ikiwa ni jumanne na ijumaa kuanzia saa 11.30 hadi saa 1.30 usiku.
Kikundi cha Mtalumbeta wakitumbuiza katika ujio wa 

Mwanzilishi na mchungaji Mkuu wa kanisa la Moto halisi (Pure Fire miracles Ministries International') mara baada alipowasili hapa nchini jijini Dar es Salaam leo.


Waumini wakanisa la Pure Fire miracles Ministries International' wakimshangilia na kumkaribisha 

Mkuu wa Kanisa hilo, Dk. Enoch Aminu kutoka nchini Ghana mara baada ya kuwasili kanisani hapo jijini Dar es Salaam.


Mkuu wa Kanisa hilo, Dk. Enoch Aminu kutoka nchini Ghana akiwapungia mkono waumini wa kanisa la Pure Fire miracles Ministries International jijin Dar es Salaam leo mara baada ya kuwasili jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mchungaji Mwenyeji, Innocent Ikechukwu. 


Mkuu wa Kanisa hilo, Dk. Enoch Aminu kutoka nchini Ghana akiwasalimia waumini wa Kanisa la Moto halisi jijini Dar es Salaam.


Mkuu wa Kanisa hilo, Dk. Enoch Aminu kutoka nchini Ghana akisalimiwa na muumini wa kanisa la Moto halisi jijini Dar es Salaam .


Mkuu wa Kanisa hilo, Dk. Enoch Aminu kutoka nchini Ghana wakimshangilia mwanzilishi wa kanisa lao mara baada alipowasili jijini Dar es Salaam.


Mkuu wa Kanisa hilo, Dk. Enoch Aminu kutoka nchini Ghana akizungumza na waumini mara baada alipowasili jijini Dar es Salaam (kulia) ni Mkalimani.


Mkuu wa Kanisa hilo, Dk. Enoch Aminu kutoka nchini Ghana akizungumza na waumini wa Kanisa la Moto halisi (Pure Fire miracles Ministries International') lilopo Tabata Segerea kwa Bibi jijini Dar es Salaam mara baada alipo wasiri hapa nchini majira ya saa 6: 30 na kuzungumza machache na waumini wa kanisa hilo kuhusu huduma atakayoitoa kwa waumini hao. 


Mkuu wa Kanisa hilo, Dk. Enoch Aminu kutoka nchini Ghana akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam mara baada ya kuwasili katika Kanisa la Moto halisi (Pure Fire miracles Ministries International') lilopo Tabata Segerea kwa Bibi jijini Dar es Salaam. 


Mchungaji Mwenyeji, Innocent Ikechukwuakizungumza wakati wa kumkaribisha Mkuu wa Kanisa hilo, Dk. Enoch Aminu kutoka nchini Ghana mara baada alipo wasili kanisani hapo jijinio Dar es Salaam.


Pia amemshukuru kwa kuitikia wito wake kuja hapa nchini kutoa huduma ya neno la Mungu pamoja na ukombozi wa Mafanikio ya wanajamii watakao hudhuria katika huduma kanisani hapo.


Baadhi ya waumini wa Kanisa la Moto halisi (Pure Fire miracles Ministries International') lilopo Tabata Segerea kwa Bibi wakimuaga Mkuu wa Kanisa hilo, Dk. Enoch Aminu kutoka nchini Ghana mara baada ya kufika na kuongea na waumini hao. 

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.