Habari za Punde

MJUE MGOMBEA URAIS TFF ALLY MAYAY MANIFESTO TEMBELE

 1. 1. UTANGULIZI Mchezo wa mpira wa miguu au soka ndio mchezo unaongoza kwa kuwa na washabiki wengi zadi duniani kuliko michezo mingine yote.  Na. MCHEZO IDADI ENEO (BARA) 1 Soka 3.5 Bill Ulaya , Afrika, Asia , America 2 Cricket 2.5 Bill Asia, Australia UK 3 Field Hockey 2 Bill Ulaya, Afrika, Asia, Australia 4 Tennis 1 Bill Ulaya, Asia, America 5 Volleyball 900 Mil Ulaya, Australia, Asia, America 6 Table tennis 850 Mil Ulaya Afrika, Asia, America 7 Baseball 500 Mil America, Japan 8 Golf 450 Mil Ulaya, Asia, America, Canada 9 Basketball 400 Mil America 10 American football 400 Mil Ulaya, Afrika, Asia, America, Australia
Mchezo wa soka nchini Tanzania kama ilivyo katika nchi nyingine unasimamiwa na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) ambalo lilianzishwa mwaka 1930 likiitwa Chama cha Mpira wa Miguu Tanganyika kabla ya kubadilishwa mwaka 1971 na kuwa Chama cha Mpira wa Miguu Tanzania. Chama hicho kilibadilishwa tena mwaka 2004 kuwa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (Tanzania Football Federation – TFF). TFF ni Mwanachama wa Shirikisho la Soka la Dunia (FIFA) na la Afrika (CAF)  tangu mwaka 1964 hivyo na kuwa na uanachama  katika mashirikisho hayo kwa Zaidi ya nusu karne.
1. 1.1.Historia ya Mafanikio Katika kipindi hiki cha zaidi ya miongo mitano, mafanikio makubwa ya soka kwa ngazi ya timu ya Taifa ni yale ya mwaka 1980 wakati timu yetu ya Taifa (Taifa Stars) iliposhiriki kwenye Fainali za Kombe la Mataifa Huru ya Afrika zilizofanyika nchini Nigeria; na pale Timu ya Taifa ya Wanawake (Twiga stars) ilipopata nafasi ya kushirikikatika fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika kwa wanawake mwaka 2010. Kwa upande wa vilabu, hali ni mbaya zaidi. Mafanikio pekee ya kutaja kwenye mashindano ya kimataifa ni pale timu ya Simba S.C ya Dar es slaam ilipofanikiwa kufika katika hatua ya fainali ya kombe la Shirikisho mwaka 1993 na kuwa mshindi wa pili baada ya kufungwa na Stella Club d`Adjame ya Ivory Coast. Pamoja na Timu za Taifa na Vilabu kutofanya vizuri kwa muda mrefu katika mashindano ya Kimataifa lakini washabiki wameendelea kufurika viwanjani kuishangilia timu zao tofauti na nchi nyingi zilizo katika eneo la Afrika ya Mashariki na Kati. Mafanikio mengine yaliyopatikana kutokana na mpira wa miguu ni ajira kwa wachezaji wa timu zinazoshiriki ligi kuu ya Vodacom Tanzania Bara. Timu hizo zimekuwa zikitoa  ajira za muda (contractual) kwa vijana wasiopungua 450 kila mwaka ambao husaini mikataba ya kuvichezea vilabu 16 vinavyoshiriki katika ligi kuu ya Vodacom Tanzania Bara.  
Dira na Malengo ya Uongozi wangu!! 1. 2. KUANZISHA NDOTO YA MAFANIKIO YA SOKA LA TANZANIA (ESTABLISHMENT OF TANZANIA FOOTBALL VISION 20….)
2. 2.1.Utangulizi Kama ilivyo kwa taifa letu ambapo tuna Dira ya Maendeleo ya Taifa iliyoanzishwa mwaka 1994 na kuibuliwa rasmi mwaka 1999 ikitupa mwongozo wa nini cha kufanya kufikia malengo ya kiuchumi na kijamii kwa Taifa itakapofika mwaka 2025. 
Kwa bahati mbaya sana, sekta ya mchezo wa mpira wa miguu/soka imekuwa ikiendeshwa bila kuwa na malengo madhubuti ya muda mrefu, wa kati na mfupi. Miongoni mwa yaliyonivuta kugombea uongozi ni haja ya kuwa Dira (vision) ambayo itaongoza sekta hii ili kufikia malengo hayo kwa muda utakaoainishwa katika dira hiyo. Mpango kama huu wa kuwa na Dira ya Maendeleo ya Soka sio mgeni na umekuwa ukitumiwa na mataifa mbalimbali na kuwezesha baadhi ya nchi kufanikiwa kupiga hatua kubwa baada ya kufanya thathmini ya kina ya uwezo wa ndani na kuweka mikakati yenye uhalisia ili kuweza kutekeleza mikakati hiyo. Baadhi ya nchi hizo ni kama vile Afrika ya Kusini, Zambia, Ujerumani, Uingereza n.k. zimefanikiwa kufikia malengo yao katika maendeleo ya soka kwa kuweka mikakati kama hii. 
Mathalan, mwezi Desemba mwaka 2014 Shirikisho la Mpira wa Miguu la Afrika ya kusini (SAFA) lilizindua Dira yake ya maendeleo ya soka ya mwaka 2022 (SAFA VISION 2022) ambapo pamoja na mambo mengine, wamejiwekea malengo kuwa ifikapo mwaka 2022, asilimia kumi ya vijana wa nchi hiyo wawe wanacheza mpira wa miguu na timu ya Taifa ya Afrika ya kusini iwe katika nafasi tatu za juu kwenye  orodha ya ubora ya CAF. 
Aidha, Dira ya Shirikisho la soka la Zambia (FAZ) ni vinara wa soka la Afrika (African Football Power house). Shirikisho la soka la nchi ya Qatar lina Dira ya 2021 yenye malengo ya kuwa chama kiongozi kwa ubunifu na ushindi.  Mwaka 2014 Chama cha soka nchini Uingereza kiliibua Dira yao (Vision 2020) yenye malengo kuwa ifikapo mwaka 2020 kuwa na vituo vya soka 150 katika miji 30 nchini humo,na pia wawe wameweza kuvutia 
uwekezaji kwenye soka wenye thamani ya jumla ya Paundi milioni 230 ndani ya miaka sita. KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

1. 3. DHAMIRA NA MIKAKATI YETU 2. 3.1. Kutengeneza Dira ya Maendeleo ya Soka nchini Naelewa fika kuwa hatua za awali kabisa baada ya kuchaguliwa kwangu lazima zilenge kwenye kuhuisha na kuanzisha mifumo thabiti ya uendeshaji wa soka hapa nchini baada ya kuvurugwa na uongozi uliomaliza muda wake. Lakini pia natambua umuhimu wa kuwa na dira ya maendeleo ya soka hivyo tunatarajia kuanzisha mchakato shirikishi ambao utapelekea kutengeneza Dira itakayaongoza utendaji wa shirikisho la mpira wa miguu  nchini chini ya utawala wangu kwa muda tutakaokubaliana. Hii italisaidia Shirikisho kupitia wadau wote wa mchezo wa soka sio tu kutathmini uongozi wangu bali pia mwenendo mzima wa soka letu  na maeneo muhimu ya kushughulikia na baadae kutoa mwongozo wa namna ya kutatua baadhi ya changamoto ili kufikia malengo tutakayokuwa tumejiwekea. Nitapendelea mafanikio au udhaifu wa uongozi wangu uje kupimwa kutokana na malengo haya kwa kuna natarajia mchakato huu utakuwa shirikishi ambapo tutajiwekea malengo na kubuni njia za kuyafikia huku kukiwa na viashiria (indicators) vinavyopimika ambavyo tutavitumia kujifanyia tathmini ya utekelezaji.
1. 3.2. Kurasimisha mpira wa miguu (Formalisation of  Tanzania Football ) Wakati inapata uhuru, Tanzania ilikuwa na watu Milioni 10  na idadi hiyo kuongezeka kila mwaka  hadi ilipofika mwaka 2015 idadi ya watanzania ilikuwa ni  48. Kwa mujibu wa Ripoti ya Mamlaka ya Takwimu Tanzania (NBS) ya mwaka 2016 Tanzania ilikuwa ina Jumla ya watu 50,144,175 huku ikionesha kuwa asilimia 43.9% ni vijana chini ya miaka kumi na tano (U-15), sawa na kusema Tanzania kuna vijana 22,013,293 walio chini ya umri wa miaka 15. Hii ni hazina kubwa sana kwa maendeleo ya mchezo wa 
soka nchini Historia inaonyesha kuwa, serikali kwa upande wake imejitahidi na kuonesha kuwa na nia ya dhati ya kuendeleza sekta hii kupitia hatua kadhaa ambazo imezichukua tangu uhuru mwa 1961. Miongoni mwa hatua hizo ni kama:• ♣ Uundwaji wa Wizara ya Utamaduni wa Taifa na Vijana mwaka 1962 na kuipa  jukumu la kuendeleza michezo nchini; • ♣ Kuundwa kwa Baraza la Michezo la Taifa mwaka kupitia sheria Na. 12 ya mwaka 1967 na kulipa jukumu la kuongoza na kuratibu maendeleo ya michezo kwa kushirikiana na vyama vya michezo. • ♣ Mwaka 1973 katika mkutano mkuu wa 16 wa TANU lilipishwa azimio lililotaka michezo ipewe kipaumbele na ionekane kuwa ni sekta muhimu katika uhai wa Taifa. Pamoja na kuwa mpaka mwaka 2016 ligi kuu ya Vodacom Tanzania Bara imeweza kutoa ajira kwa vijana 480 ambao wamesajiliwa na timu zinazoshiriki katika ligi hiyo huku wakiendesha maisha yao kupitia kazi ya kucheza mpira wa miguu,  bado mchango unaotolewa  na mchezo wa soka katika maendeleo ya kiuchumi na kijamii bhaujatambuliwa kuwa ni mkubwa kiasi cha kuutengenezea mkakati wa pamoja kati ya serikali na wadau wengine ili kuweza kusaidia maendeleo ya sekta hii muhimu  inayotoa ajira nyini kwa vijana. Hili limechangiwa sana na udhaifu wa kiuongozi kwenye Shirikisho la Mipra wa Miguu na hili ni jambo moja la muhimu ambalo uongozi wangu utapigana kulibadilisha. Tutaandaa mpango mkakati utakaowasilishwa serikali kuiomba erikali kurasimisha mchezo wa mpira wa miguu na kuwa sekta iliyo rasmi kama zilivyo sekta nyingine kwenye uchumi. Mpango huo utathibitisha kinagaubaga mchango wa soka wa moja kwa moja na kupitia kwa wadau 
kwenye pato la taifa na Maendeleo ya kijamii kwa jumla.

1. 4. KUANDAA MPANGO WA PAMOJA (JOINT STRATEGY ) KWA KUSHIRIKIANA NA SERIKALI  KATIKA KUJENGA NA KUENDELEZA MIUNDOMBINU YA MCHEZO WA SOKA 2. 4.1. Utangulizi Ukuaji wa miji na miji  na majiji umekuwa   ukiongezeaka kutokana ongezeko la idadi ya watu mijini hasa ukizingatia kuwa  kwa mujibu wa ripoti ya NBS ya mwaka 2016 inayoonesha kuwa  wastani wa kuogezeka kwa idadi ya watu tanzania ni asilimia 3 % tangu mwaka 2010  hivyo ina maana kuna zaidi ya watu milioni m1.5 huongezeka kila mwaka nchini Tanzania.  Ongezeko hili la watu mijini haliendani na uwekezaji katika miundombinu ya miji na majiji ikiwemo maeneo ya wazi na viwanja vya kuchezea. Nchu yetu ni moja kati ya nchi wanachama wa Shirika shirika la Umoja wa mataifa la UNESCO linalotambua  haki za watoto ikiwepo haki ya kucheza .Article 31 ya UNICEF (Leisure, play and culture) Children have the right to relax and play, and to join in a wide range of cultural, artistic and other recreational activity na sheria ya haki za watoto ya Tanzania ya mwaka 2009 inayotambua haki ya kucheza ya mtoto lakini bado utaratibu wa mipango miji katika maeneo mbali mbali ya nchi yetu hauzingatii umuhimu wa kuacha maeneo ya wazi  kwa ajili ya michezo mbalimbali kwa watoto ukiwepo mchezo wa mpira wa miguu. 1. 4.2. Changamoto Kutokuwepo kwa maeneo au viwanja vya kucheza mpira kwa vijana katika maeneo ya kuishi na mashuleni ni moja kati ya changamoto kubwa inayopeleka vijana wengi wenye vipaji kukosa fursa ya kuendeleza vipaji vyao. Ukuaji wa miji na majiji pamoja na ongezeko la idadi ya watu mijini haliendi sambamba na ujenzi wa miundombinu  na uachaji wa  wa maeneo ya wazi kwa ajili ya michezo  kwa vijana katika miji mipya 

1. 4.3. Dhamira yetu/Mkakati Kwa kushirikiana na Serikali baada ya kuona mchango wa mchezo wa soka katika Maendeleo ya kiuchumi na kijamii, tutaanda mpango kwa kushirikiana na Serikali wa kuweka vivutio kwa wawekezaji  watakaowekeza katika miundombinu ya michezo pamoja na vifaa vya kujifunzia kama vile  viatu, jezi za watoto ili wadau wengi waweze kumudu gharama hizo.  
1. 5. KUANDAA  MIKAKATI YA KUSHIRIKIANA NA BAADHI YA MATAIFA  RAFIKI (DEVELOPMENT PARTNERS) 2. 5.1. Utangulizi Nchi yetu ni moja kati ya nchi zenye nchi marafiki wengi duniani kihistoaria kutokana na msimamo wa siasa zisizofungamana na upande wowote wakati wa vita baribi. Mahusiano haya na baadhi ya mataifa yamekuwa na faida nyingi za kijamii na kiuchumi ikiwepo 1. 5.2. Changamoto Mpaka sasa licha ya kuwa na makubaliano ya ushirikiano na mataifa mbalimbali rafiki  nan chi yetu katika sekta mbalimbali  bado hatujathubutu  kupendekeza kuwa na ushirikiano  katika maeneo ya michezo na utamaduni  kati ya nchi yetu na mataifa rafiki . 1. 5.3. Dhamira yetu/Mkakati Kupitia maafisa   Ofisi zetu za Ubalozi katika nchi marafiki zetu ambazo zinaeleweka kuwa na uwezo wa kutusaidia katika maeneo ya technical assistance, financial assistance, tutaishawishi Serikali kupitia ofisi zetu kujenga mahusino na Mahirikisho ya soka ili kupata nafasi ya kubadilishana uzjuzi na uzoefu. Nchi kama Uholanzi, Sweden, German, Denmark, Uturuki, China , India, Brazil, Morocco, Misri, Algeria , Tunisia na  Afrika ya Kusini  zinaweza kuwa washirika wetu wakubwa wa karibu katika 
maendeleo ya pamoja  ya  mchezo wa soka.
1. 6. UTAWALA 2. 6.1. Utangulizi Msingi wa mafanikio ya  nchi, shirika au  Taasisi yoyote  ni uwepo  wa watumishi bora na mfumo rafiki wa kuwatumia watumishi ili kufikia malengo ya Taasisi husika. (Human resource). Watumishi bora hupatikana kupitia uwepo wa misingi ya utawala bora katika Taasisi husika. 6.2. Dhamira yetu/Mkakati Kusimamia misingi ya utawala bora katika utekelezaji wa mjukumu ya kila siku kwa kuwepo kwa semina za mara kwa mara ili kwajengea uwezo wafanyakazi katika nyanja mbalimbali. Misingi hiyo ni pamoja na:• • Uwazi:  kuendesha shughuli za mpira wa miguu bila usiri na kificho ili wadau wawe na uwezo wa kupima utendaji na uzingatiaji wa kanuni, taratibu na sheria . Kuwepo kwa uwazi kwa fedha za misaada kutoka kwa FIFA, CAF na wafadhili wengine. • • Uwajibikaji: ni kiongozi/mtendaji kuwa tayari kujibu, kubeba dhamana na kutoa maelezo kwa wadau wa soka juu ya maamuzi au matendo aliyoyafanya katika kutekeleza dhamana aliyopewa. • • Utawala wa sheria : usawa mbele ya sheria kwa watu wote • • Ushirikishwaji: kuwahusisha wadau wa makundo yote katika kufanya maamuzi yanayowahusu • • Usawa: kutoa fursa sawa kwa wadau  ya kushiriki katika 
mambo yanayowahusu  kwa munufaa yao • • Ufanisi na tija: hali ya utendaji inayozalisha matokeo yanayokidhi malengo na matarajio ya watu na jkuhakikisha matumizi mazuri ya rasilimali • • Mwitikio: kutoa huduma kwa jamii kwa wakti na katika kiwango kinachokidhi matarajio ya watu. • • Maridhiano: kukutanishwa kwa mawazo mbalimbali ili kupata suluhu au maamuzi ya pamoja ambayo yanazingatia matakwa ya jamii nzima. • • Uadilifu : hali ya kuwa mwaminifu na mwenendo mzuri katika utendaji wa kazi Kuongeza idadi ya washiriki (Uwakilishi wa washabiki & wadhamini katika sehemu za maamuzi 
1. 7. MIUNDOMBINU YA MCHEZO WA SOKA(VIWANJA) 2. 7.1. Utangulizi Miundo mbuni ya mchezio wa soka ikiwemo viwanja vya kuvhezea ni moja katia ya vitu vya msingi katika maendeleo ya mchezo wa soka. Ndio maana katika sgeria 17 zinazotawala mchezo wa sioka, sheria namba mojani uwanja wa kuchezwea kwani bila ya kuweponkwa uwanja wa kuchezea hakuwezi kuw ana mchezio wenyewe hivyo  uuwepo  wa  uwanja/viwanja vya kuchezea ndio msingi  wa mipango yote ya maendeleo katika mchezo wa soka. Tanzania tumefanikiwa na viwanja  katika kila makao makuu ya Mkoa ambavyo vinamilikiwa na Chama cha Mapinduzi  huku Mikoa mipya kama vile Songwe, Geita ikiwa haina viwanja vya ukubwa kulingana na 
mahitaji ya sasa. Aidha jijini Dar es Salaam kuna viwanh Ja vinne ambavyo vinaweza kutumika kwa mechi za ligi kuu huku viwili katia ya hivyo ndivyo vyewe uwezo kutumima wakati wa Usiku (Taifa, Azzam Complex). Hivyo changamoto ya viwanja vya kuchezwea mechi na vya kufanyia mazoezi inaendelea kuwepo katika Miji na Majiji ya Tanzania. 1. 7.2. Changamoto Ongezeko la idadi ya watu ni moja kati ya changamoto kubwa katika upatikanaji wa huduma zinazoendana na ongezeko hilo katika nchi nyingi zinazoendelea ikiwemo nchi yetu pendwa Tanzania. Kwa mujibu wa Ripoti ya sense ya makzi ya watu iliyofanbtika mwaka 2012, Tanzania inaonekana kuwa na ongezeko la asilimia 3% kila mwaka (population growth rate) . 1. 7.3. Dhamira yetu/Mkakati Kushirikiana na Serikali kuhakikisha kila wilaya inapoandaa ramani ya mipango mji kuzingatia uwepo wa maeneo ya wazi kwa ajili ya michezo ya watoto. Maeneo ya wazi ni muhimu kwa kuwa katika maeneo ya wazi kwenye makazi ya watu  ndipo mahali ambapo  watoto wadogo  huanzia kucheza soka la mitaani kabla ya kwenda katika viwanja vya mashule ambavyo pia mashule mengi ya mijini hayana maeneo ya viwanja vya kuchezea Aidha, kila chama cha mkoa kuomba eneo la wazi kwa ajili ya uwanja wa mpira ,  upatikanaji wa fedha  za kulipia maeneo hayo zitajadiliwa katika Vikao vya kamati ya fedha na kamati tendaji. 
1. 8. MCHEZO WA SOKA /WANACHAMA 2. 8.1. Wadau wa soka (Stakeholders) (Stakeholders) wa mchezo wa soka ndio watu muhimu katika maendeleo ya mchezo wa soka Duniani kote hasa ukizingatia kuwa mchezo wa soka ni mchezo unaovuta hisia za watu wengi zaidi Duniani kuliko michezo 
mingine. Katiba yetu ya TFF  inayotuongoza inatambau umuhimu wa wadau wa mchezo wa soka imeelezea wanafanamilia wa mpira wa miguu kuwa ni wale tu wenye kuhusika moja kwa moja na uongozi katika vilabu na Shirikisho  na wanachama wake lakini wadau  wa soka ni zaidi ya viongozi na wanachama waliotamkwa katika katiba ya TFF. Uwepo wa utaratibu wa kuwatambua wanafamilia wa mchezo wa soka na uwepo wa taratibu za kushughulikia maswala mbali mbali ya kisheria kuhusu mchezo wa soka na utaratibu mzima uliotengenezwa wa kusimamia maswala ya kisheria, kikanuni na kimaadili kusimamiwa na wanafamilia wenyewe ndani ya mfumo wa soka umesaidia katika kuujenga na kuufanya mchezo wa soka kuwa maarufu zaidi na kuendelea kuwa mchezo wa kipekee sio tu Afrika bali Duniani kote. Hivyo wadau   kama vile wafadhili  na washabiki ambao ndio msingi wa maendelo ya mchezo wa soka kutokuwemo katika tafsiri ya wanafamia ni moja katia ya maswala ambayo yanatakiwa kupewa kipaumbele  hasa ukizingatia kuwa wadau hawa ndio msingi wa maendeleo ya mchezo wa soka. Hivyo  utaratibu unatakiwa kuangaliwa upya ili kuona umuhimu wa uwepo wa wawakilishi wa  wadau muhimu katika  sehemu za maamuzi ili kublinda maslahi yao. Hivyo tutaangalia namna  bora ya kutanua wigo wa uwakilishi kwa wadau muhimu kama vile wadhamni ,  wafadhili na washabiki waliopo katika mchezo wa soka kuwemo katika sehemu za maamuzi  ili kupata fursa ya kuwa na mitazamo tofauti katika vikao vya maamuzi  kuhusu maendeleo ya mpira wa miguu nchini 1. 8.2. Soka la Wanawake Ni moja kati ya tunu tuliyonayo katika mchezo wa soka hasa ukizingatia kuwa mafanikio kidogo kimataifa tuliyopata ni sababu tosha inayoonesha hazina yuliyonayo katika soka la wanawake.  Ligi ya soka la Wanawake iliyoanzishwa mwaka huu 2017 inaweza kuwa na mchango mkubwa katika maendeeo ya soka la Wanawake. Kwa kushirikiana na TWFA tunahitaji kuhamasisha wanawake /vijana nchini kucheza na kuunga mkono soka la 
wanawake kwani uwezo wa kushiriki michuano ya kimataifa kwa soka la wanawake umekwishaonekana. Mpango wa uhamasishaji mkoa kwa mkoa unatakiwa kufanyika ili kuhakikisha mikoa yote ya Tanzania inachezwa soka la wanawake. Ligi ya wanawake iliyoanzishwa inatakiwa kusimamiwa vema  ili kuvutia wanawake wengi zaidi katika soka huku jihudi za kupata wadhamini wengine zikiendelea kwa ajili ya kuboresha maeneo mbalimbali .
1. 8.3. Soka la ufukweni Soka la ufukwen ni mchezo mpya kwa watanzia walio wengi hivyo inahitaji nguvu ya ziada kutumika katika kuutangaz amchezo huu hasa ukizingatia kuwa nchi yetu ni moja kati ya nchi zenye Pwani yenye urefu mkubwa katika bahari ya hindi, inayokadiriwa kuwa na urefu wa km  800 hivyo kutokuwa na changamoto ya kutafuta viwanja vya mazoezi kama ilivyo kwenye baadhi ya nchi ambazo hazina pwani.
1. 8.4. Ligi za Taifa Tuanatakiwa kuwa na makakati wa kurejesha washabiki wa soka viwanjani kwani takwimu zinaonesha kuwa idadi ya mashabiki wanaoin gia viwanjani inazidi kupumngua siku hadi siku, tofauti na miaka ya nyuma ambapo mechi zote za ligi daraja la kwanza, la pili, la tatu na la nne zilikuwa zinajaza watu viwanjani. Maneo yatakayozingatiwa katika mkakati huu ni   maeneo makuu matatu ambayo ni:a. i. Kuongeza ushiriki wa vilabu katika usimamizi wa sheria na kanuni za mshindano ili kuongeza uwazi katika maamuzi na  kupunguza au kuondoa  kabisa malalamiko kwa vilabu vinavyoonekana kuwa ni vidogo. b. ii. Kutumia weledi katika maswala ya masoko na utawala (Marketing & administration) kwa ajili ya kusimamia na kutangaza 
ligi zetu ndani na nje ya nchi. c. iii. Kuongeza program za kuwajengea uwezo (capacity building programs) viongozi wa vilabu na shirikisho/bodi ya ligi katika maswala mbalimbali kama vile masoko, utawala n.k ili kuivijengea uweo vilabu kuweza kumudu gharama za uendeshaji wa timu.  Ligi za Taifa(Ligi kuu na ligi daraja la kwanza)  zinatakiwa kuendea kuboreshwa na hasa kuongeza uwazi na  fursa kutolewa kwa vijana wenye weledi na wabunifu ili waweze kubuni mbinu za kuitangaza zaidi na kuweza kuibua vyanzo vipya vya fedha mbali na viingilio na mauzo ya haki za matangazo ya Televisheni. Aidha weledi unatakiwa kuongezeka katika uendeshaji wa ligi katika maeneo yote kuanzia Utawala, uamuzi, ufundishaji hadi uchezaji ili kuongeza tija na kuvutia watu ambao wengi wao wamekuwa wakivutiwa kuangalia  mechi za ligi mbalimbali barani Ulaya.
1. 8.5. Ligi za Mikoa Vyama vya mikoa ambavyo ndio vinavyosimamia ligi za mikoa vitahitaji kupitia upya utaratibu wa kuendesha na mashindano hayo na hasa gharama zinazoambatana na mashindano ikiwepo malipo kwa waamuzi na viwanja. Kila mkoa utatakiwa kuandaa mpango wake wa maendeleo wa mkoa utakaojumuisha Wilaya zake zote. Aidha kila Mkoa kwa kushirikiana na sekretarieti ya TFF utawasilisha rasimu ya mpango na vyanzo vya mapato yanayotumika kugharamia shughuli za uendeshaji wa  ligi. Lengo ni kuweza  kupitiwa na wataalamu ili kuboresha utaratibu huo na kuweza kuvifanya vyama vya mikoa kumudu gharama za mashindano hayo ikiwemo kutoa semina na mafunzo  kwa waamuzi kabla ya mashidano yoyote ya mkoa na wilaya kuanza.
1. 8.6. Wachezaji Ni eneo muhimu linahitaji kupewa uzito wa kipekee hasa kubadilisha mitazamo ya wachezaji wa ndani juu ya kutafuta nafasi ya kucheza soka la kulipwa nje ya nchi. Utaandaliwa utaratibu wa kusaidia kupata timu za kuchezea nje ya nchi na kuhimiza wachezaji vijana kutoka nje ya nchi kukliko kubakia katika vi;labu vya Tanzania. Semina elekezi kwa wachezaji zitatolewa mara kwa mara ili kutoa elimu hiyo. Wachezaji wa zamani wanatakiwa kutumika katika maeneo mbalimbali ya mchezo wa soka na kuhakikisha wanajengewa uwezo katika maeneo ya uongozi na ualimu/ ukocha wa mpira wa soka. 
1. 8.7. Makocha Ni wadau muhimu kwa Maendeleo ya mpira wa miguu hasa makocha maalum wa kufundisha soka la vijana (youth football coaches). Kila mkoa , Wilaya unatakiwa kuwa na idadi maalum ya makocha wa ngazi tofauti kulingana na mahitaji ya mkoa/wilaya hiyo. Zoezi la tathmini linatakiwa kufanyika ili kujua mahitaji halisi na kupanga makakati wa kufikisha idadi ya makocha tarajiwa.Vyama vya makocha katika Mikao na Wilaya vinatakiwa kujengewa uwezo wa kusimamia makocha katika ngazi hiyo ili kurahisisha utendaji katika ngazi ya Taifa.Usimamizi wa  makocha unatakiwa kuwa chini ya maocha wenyewe hasa waliostaafuu ambao wanatakiwa kufanya kazi ya  kusaidia katika kuwasimamiam wamakocha wa sasa. Kozi mbalimbali za ndani na n je ya nchi  zinatakiwa kutolewa na jitihada zinatakiwa kufanyikan ili makocha wetu watoke nje ya nchi ili kuwajengea uwezo za uzoefu wa kufundisha soka katika mataifa mbalimbali Duniani .
1. 8.8. Waamuzi Ni wadau muhimu kwa Maendeleo ya mpira wa miguu ambao wanatakiwa kuangaliwa na kujisimamia wenyewe hasa ukizingatia kuwa wapo waamuzi 

wengi wastaafu ambao bado hawajatumika ipasavyo katika kuzalisha waamuzi wapya mahiri na kuwasimamia.  Mafunzo ya mara kwa mara kwa waamuzi katika ngazi mbalimbali yanatakiwa kufanyika  kwa kutumia waamuzi wastaafu ili kukidhi mahitaji ya waamuzi katika kila Wilaya/Mkoa nchini. Idadi ya waamuzi na madaraja yao inatakiwa kufahamika kuanzia katika Ngazi ya Wilaya, Mkoa, hadi Taifa.Vyama vya waamuzi katika ngazi za Wilaya/Mikoa vinatakiwa kujengewa uwezo ili kuweza kusimami tasnia hiyo kuanzia katika ngazi ya chini na kurahishisha utendaji wao katika ngazi ya Taifa.

1. 8.9. Madaktari wa tiba michezoni Ni wadau muhimu kwa Maendeleo ya mpira wa miguu hasa ukizingatia kuwa mpira wa miguu unahitaji utimamu wa mwili ili mchezaji aweze kutekeleza majukumu yake uwanjani. Mafunzo ya FIFA/CAF ya  tiba za wanamichezo yanatakiwa kufanyioka mara kwa mara na katika kila kona ya nchi yetu ili kuweza kuwaandaa wachezaji wetu lakini pia kupata ushauri na tiba stahili pale wanapopata ajali mchezoni ili wasipoteze vipaji vyao. 
1. 8.10. Vyama vya  Mikoa na Wilaya Kuandaa platform ya mawasiliano ya moja kwa moja kati ya makatibu wa mikoa na katibu Mkuu wa TFF kupitia mfumo wa kielektroniki utakaomwezesha  Katibu Mkuu wa TFF kufuatilia utendaji wa kila siku wa vyama vya Mikoa kulingana na program wanazotekeleza.Kuwa  na mkakati wa kuandaa  program za mikoa na wilaya na kutoa ripoti ya utekelezaji wa program za maendeleo kila baada ya miezi mitatu kwa katibu Mkuu wa TFF. Kungalia namna ya kufikisha msaada wa fedha za maendeleo kwa wanachama wake nchi nzima katika program za maendeleo. Aidha Vyama vya mikoa  vinatakiwa kubuni vyanzo vya mapato ili kuviwezesha  kumudu gharama za  uendeshaji wa ofisi za kila siku. 
1. 8. 11 MAANDALIZI YA  YA FAINALI ZA CAF ZA U-17 ZA MWAKA 2019 NCHINI TANZANIA Ni faida kubwa kuwa wenyeji wa michunao hii ya  fainali za vijana wenye umri chini ya miaka 17 kwa kuwa tutapata nafasi ya kuingia moja kwa moja ktika fainali hili kupitia sifa hiyo ya kundaa ingawa changamoto pekee iliyopo ni kutokucheza mechi za mashindano za  awali  za kukata tiketi ya  kushiriki katika fainali hizo. Mkakati a. Mwaka 2015 walichaguliwa vijana wenye umri chini ya miaka 13 na kutengeneza kikosi cha vijana kwa ajili ya kuandaa timu ya U-17 ya mwaka 2019. Vijana hao wapo katika kituo cha Alliance jijini Mwanza wakiendelea na masomo pamoja huku wakipata mafunzo ya mpira wa miguu katika kituo hicho. Kuwaandalia programu maalum ya kuwaweka pamoja ikiwemo mashindano ya vijana wenye umri chini ya miaka 15 mweze disemba 2017 na mashindano ya vijana wenye umri chini ya miaka 16 mwaka 2018 kabla ya kufika mwaka 2019. b. Katika mashindano hayo vijana watakaoonekana wanafaa watajumuishwa katika kikosi hicho na kuendelea na program itayopangwa na benchi la ufundi. c. Mkakati wa fedha za kuendesha program hii ya miaka mitatu utasimamiwa na Shirikisho kwa kushirikiana na serikali pamoja na wadau wengine ambapo uwazi katika mahitaji na matumizi ya fedha  ndio utakuwa  msingi wa uendeshaji wa program hii. d. Tathmini ya mahitaji ya miundombinu (viwanja vya mechi na mazoezi ) kwa ajili ya fainali za u-17 za mwaka 2019 itafanyika chini ya uratibu wa kamati ya ufundi na kamati ya mashindano  pamoja na serikali ili kujua mahitaji halisi ya viwanja na ubora 
utakaokidhi  mahitaji ya CAF. e. Mashindano haya tunatakiwa kuyatumia sio kutangaza tu wachezaji wetu bali hata kutangaza vivutio vingine vilivyopo nchini  kwa kuwa tunatarajia mkuwa na mataifa nane (8) kutoka katika bara la Afrika na vyombo vya habari  vikubwa vyote vitaripoti mashindano haya hivyo ni fursa pia kwa makampuni na  wafanyabiashara wa Tanzania  kutangaza bidhaa zao kupitia  fainali hizi za U-17 za mwaka 2019. 
MWISHO Nashukuru sana kwa ushirikiano wenu! Mungu Ibariki Tanzania, Mungu Ibariki Tanzania

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.