Habari za Punde

MKUU WA MKOA LINDI ZAMBI APIGIA DEBE KILIMO CHA UFUTA NA MIHOGO

 Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Bw. Godfrey Zambi akizungumza na ugeni kutoka Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania wakati walipomtembelea ofisini kwake mjini Lindi.
 Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TADB, Bw. Francis Assenga akizungumza na Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Bw. Godfrey Zambi (hayupo pichani) wakati walipomtembelea ofisini kwake mjini Lindi.
 Mkurugenzi wa Mikopo na Biashara wa TADB, Bw. Augustino Matutu Chacha (aliyesimama) akiwasilisha mada juu ya fursa za mikopo zinazotolewa na Benki ya Kilimo kwa Wadau wa Korosho na Ufuta Mkoa wa Lindi uliofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Lindi.
 Wadau wa Korosho na Ufuta Mkoa wa Lindi uliofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Lindi.
 Wadau wa Korosho na Ufuta Mkoa wa Lindi uliofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Lindi.
Wadau wa Korosho na Ufuta Mkoa wa Lindi uliofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Lindi.
**************************************
Na Mwandishi wetu, Lindi
MKUU wa Mkoa wa Lindi, Godfrey Zambi ameiomba Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) kukopesha wakulima wa mazao ya ufuta na mihogo ili waweze kulima kilimo cha kisasa na cha kibiashara hasa kwa wakulima wadogo wadogo wa mkoani humo.
Bw. Zambi alitoa wito huo wakati wa mkutano wa Wadau wa Korosho na Ufuta Mkoa wa Lindi uliofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Lindi.
Bw. Zambi alisema kuwa mkoa wa Lindi ni mkoa uliojaaliwa katika kuzalisha mazao ya ufuta na mihogo lakini changamoto kubwa ni mtaji wa kulima kibiashara ili kukidhi mahitaji ya soko la ndani na nje ya nchi.
“Wakulima wa mkoa wa Lindi wapo tayari kushiriki katika kuleta mapinduzi ya Kilimo kutoka kilimo cha kujikimu kwenda cha kibiashara lakini kwa sasa suala la mtaji wa kilimo cha kibiashara ni changamoto kubwa,” alisema Bw. Zambi.
Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TADB, Bw. Francis Assenga alisema kuwa Benki ya kilimo ipo tayari kutoa mikopo kwa wakulima wadogo wadogo waliokuwa kwenye vikundi ili waweze kukopeshwa.
Bw. Assenga aliongeza kuwa Benki ya Kilimo pia ipo tayari kuwekeza kwenye miradi ya maendeleo ya Kilimo kwa kuipatia mikopo yenye riba nafuu zilizo chini ya viwango vya kibiashara kwenye soko.
“Kwa kutambua umuhimu wa wakulima wadogo wadogo nchini TADB imedhamiria na kujizatiti kuhakikisha inachangia kwa kiasi kikubwa katika  kuleta Mapinduzi yenye tija katika Sekta ya Kilimo nchini kwa kusaidia upatikanaji na utoaji wa fedha ikiwa ni pamoja sera nzuri zitakazosaidia maendeleo ya kilimo nchini,” alisema.
Naye, Mkurugenzi wa Mikopo na Biashara wa TADB, Bw. Augustino Chacha alisema kuwa TADB inalenga kuongeza upatikanaji wa huduma zisizo za kifedha kwa wakulima kama vile kujengewa uwezo juu ya uandaaji wa andiko la miradi ya Kilimo, pamoja na upatikanaji wa taarifa za masoko, usimamizi wa biashara, mafunzo juu ya miradi ya Kilimo na mbinu za majadiliano ya mikataba.
 “Tupo tayari kutoa mikopo kwa ajili ya kuwanyanyua wakulima kama ilivyolengwa na Serikali kupitia mikopo ya pembejeo kuongeza tija kwenye uzalishaji, miundo mbinu ya umwagiliaji na ununuzi wa zana za kilimo,” alisema.
Bw. Chacha aliongeza kuwa kwa upande wa mikoa ya kusini Benki ya Kilimo imejipanga kueendeleza miundombinu ya umwagiliaji na maghala pamoja na uzalishaji wa mbegu bora za mazao ya korosho na mihogo na kuimarisha viwanda vya kubangua mazao ya korosho, na kusindika ufuta, mihogo.
Bw. Chacha aliongeza kuwa Benki imejipanga kuwezesha uanzishaji wa mashamba mapya na ya kisasa ya mihogo, korosho na ufuta mkoani Lindi.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.