Habari za Punde

MKUU WA MKOA PAUL MAKONDA KUHUDHURIA TAMASHA LA WANAMUZIKI DAR

MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda anatarajia kuhudhuria Tamasha la wanamuziki litalofanyika Jumamosi hii katika Ukumbi wa NSSF, Dar es Salaam.

Tamasha hilo la utoaji wa elimu kwa wasanii juu ya kujiunga na mfuko wa bima limeandaliwa na Taasisi ya Muziki Tanzania (TAMUFO) kwa kushirikiana na Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF).
Akizungumza Dar es Salaam jana, Mratibu wa Tamasha hilo, Stella Joel amesema kuwa tamasha hilo litatoa fursa mbali za kiuchumi kwa wanamuziki mbalimbali nchini.
Alisema taasisi hizo zimeandaa tamasha hilo kwa kuona changamoto mbalimbali za makazi na bima zinavyowakumba wasanii wa muziki.
Alisema tamasha hilo litasaidia wanamuziki kimuziki na maisha yao kwa ujumla hali inayopelekea kukata tamaa na vipaji kufikia malengo yao ikiwemo kumiliki nyumba katika kipindi kifupi cha kazi zao.
Alisema moja ya fursa zinazotarajiwa kutolewa siku hiyo ni pamoja kuwawezesha wanamuziki kupata viwanja, nyumba pamoja na mafao ya Bima ya Afya.
“Nawasihi wanamuziki, waimbaji na wadau wote wa muziki kufika katika mkutano huu muhimu ili sisi kama TAMUFO tuweze kutimiza kusudi letu la kuwasaidia. Tunaamini tutainua maisha ya wanamuziki wetu nchini," alisema Stella.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.