Habari za Punde

MWANARIADHA SIMBU NA WENZAKE WAPOKELEWA KWA SHANGWE NCHINI


 Mwanariadha aliyeibuka na Medali ya Shaba katika mashindano ya Dunia ya London Marathon, Felix Simbu (wa pili kushoto) akiwa na wenzake wakiwa na Bendera ya Taifa wakati wakiwasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, jijini Dar es Salaam, jioni ya leo wakitokea nchini Uingereza kushiriki mashindano hayo yaliyomalizika hivi karibuni.

******************************************
Na Ripota wa Mafoto Blog,Dar
MSHINDI wa tatu wa Mbio za Dunia za London Marathon mwaka huu, Felix Simbu amesema kuwa ushindi huo alioupata si wapeke yake bali wa wanariadha wote ambao walienda kushiriki kutokana walijitoa muhanga hadi kufanya vizuri.
Simbu alishika nafasi ya tatu katika mbio za Km 42 na kuitoa kimasomaso Tanzania ambayo ilikuwa haijafanya vizuri katika mashindano hayo kwa miaka mingi.
Akizingumza na Mtandao huu wa www.sufianimafoto.com,  baada ya kuwasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa akitokea nchini Uingereza na kupokelewa na mamia ya mashabiki, Simbu alisema haikuwa kazi rahisi kupata medali hiyo imetokana na wao kujitoa muhanga.
"Ushindi huu si wangu peke yangu bali ni wa wetu sote kutokana tulikuwa na umoja."Huu ni ushindi wa wote, hivyo umoja wetu utazidi kujitahidi kufanya vizuri zaidi hapo baadae," alisema.
Alisema, aliona kama maajabu kwa ushindi huo baada ya kuona bendera ya Tanzania inapandishwa kuashiria ushindi wake.Awali, Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Harryson Mwakyembe alisema ushindi huo umewafanya Watanzania wawe na furaha kutokana hawakuwa na imani ya kufanya vizuri.
Alisema ni wakati sasa wa kuwekeza katika mchezo huo ili uweze kupiga hatua zaidi. Simbu aliwasilia saa 12:20 jioni kutokana na kuchelewa kufika ambapo awali aliyatarajiwa kufika saa 6:05 mchana.
Kufika kwake alipokelewa na vikundi mbalimbali vya ngoma, wasanii ambao waliongozwa Khadija Kopa na Riyama Ally.

 Simbu akikabidhiwa Uwa na mkewe, Rehema Daud, wakati wa mapokezi
 Mfanyakazi wa DsTv, Salma na wenzake nao walikuwa ni miongoni mwa mashabiki wa Simbu waliofika kumpokea, huku wakipiga picha za kumbukumbu kwa simu.
 Simbu akipokelewa na mashabiki wake akiwa amembeba mtoto wake
 Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe, akizungumza wakati wa hafla ya mapokezi hayo iliyofanyika kwenye Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere.
Katibu Mkuu wa Chama cha Riadha Tanzania, Gida Budai akizungumza, wakati wa hafla hiyo 
 Brigedia Gen JJ Mbungo, akizungumza na kutoa salamu kwa niaba ya Mkuu wake 
 Sehemu ya wageni waliohudhuria mapokezi hayo pamoja na waandishi wa habari wakiwa kazini
 Mwanariadha Felix Simbu akionyesha Medali yake kwa Waziri Mwakyembe
 Wazori Mwakyembe akionyesha Medali hiyo baada ya kuonyeshwa na Simbu
 Wazazi wa mwanariadha huyo, Baba Felix Simbu na Mama Salome Ntandu wakionyesha na kufurahia Medali ya mtoto wao. 
 Wanariadha hao wakimkabidhi Bendera ya Taifa Waziri Mwakyembe baada ya kukamilisha kazi waliyotumwa na Taifa
 Familia ya mwanariadha huyo 
 Baadhi ya wasanii wakiongozwa na Khadija Kopa na Riama, wakifurahia wakati wa mapokezi hayo.
 Ilikuwa ni shangwe tu wakati wa mapokezi hayo
 Hakuna aliyekaa kimya bila kumshangilia Simbu wakati akitokeza kwenye geti la Uwanja huo.
Katibu akibebwa na kucheza na baadhi ya wanariadha.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.