Habari za Punde

SERIKALI YAPOKEA GAWIO LA SH. BILIONI 19.5 KUTOKA BENKI YA CRDB


 Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mlipaji Mkuu wa Serikali Bw. Doto James (wa tatu kushoto) akipokea mfano wa hundi ya Sh. bilioni 19.5 kutoka kwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa CRDB, Bw. Ally Laay, ikiwa ni gawio kwa Serikali kutoka Benki ya CRDB, hafla iliyofanyika katika ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango, Jijini Dar es Salaam.
 Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya CRDB Dkt. Charles Kimei (kushoto), akizungumza na Waandishi wa habari wakati wa hafla ya kutoa gawio kwa Serikali kiasi cha Sh. bilioni 19.5, zinazotokana na asilimia 21 za hisa za Serikali zilizowekezwa kwa kushirikiana na Serikali ya Denmark kwenye Benki hiyo ambazo Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Doto James amesema zitaelekezwa kwenye Sekta ya Afya.
 6553
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dkt. Charles Kimei (katikati) akitoa maelezo kuhusu gawio la shilingi bilioni 19.5 ambazo benki yake imeikabidhi Serikali kutokana na kuwa mbia wa Benki hiyo kupitia fedha zilizowekezwa  ikiwa ni msaada uliotolewa na Serikali ya Denmark ili kuijengea uwezo Benki hiyo miaka ya 1994.
Baadhi ya waandishi wa Habari Jijini Dar es Salaam wakiwa katika hafla ya Serikali kupokea gawio la Sh. bilioni 19.5 kutoka Benki ya CRDB, linalotokana na uwekezaji wa asilimia 21 za hisa zote za Benki hiyo, katika ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango Jijini Dar es Salaam.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Doto James akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusu ushiriki wa Benki ya CRDB katika kuliletea Taifa maendeleo ya kiuchumi, wakati wa hafla ya kupokea gawio la Sh. bilioni 19.5 kwa niaba ya Serikali, katika ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango Jijini Dar es Salaam.  Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini-Wizara ya Fedha na Mipango.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.