Habari za Punde

SIMBA SC YAONYESHA BUNDUKI ZAKE KUELEKEA MCHEZO WA NGAO YA HISANI AGOST 23,YAICHAPA RAYON 1-0

 Mshambuliaji mpya wa Simba SC, Haruna Niyonzima, akiruka kukwepa kwanja la beki wa Rayon Sport Fc ya Rwanda, Azyisenga Jean D'amour, wakati wa mchezo wa kirafiki katika maadhimisho ya sherehe za utambulisho wa wachezaji wapya wa Klabu ya Simba 'Simba Day'. uliochezwa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, leo jioni  Katika mchezo huo Simba ilishinda bao 1-0 lililofungwa na Mohamde Mo katika dakika ya 16 kipindi cha kwanza. Picha zote na Muhidin Sufiani (MAFOTO)
 Niyonzima akimtoka beki wa Rayon Sport Fc
 Mshambuliaji wa Simba SC, John Bocco, akiruka kukwepa kwanja la beki wa Rayon Sport Fc ya Rwanda Mugabo Gabriel, wakati wa mchezo wa kirafiki katika maadhimisho ya sherehe za utambulisho wa wachezaji wapya wa Klabu ya Simba 'Simba Day'. uliochezwa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam,leo jioni.
 Mohamed Mo, akiifungia timu yake bao
 Wanenguaji wa bendi ya African Stars, 'Twanga Pepeta', wakitoa burudani wakati wa mchezo wa kirafiki katika maadhimisho ya sherehe za utambulisho wa wachezaji wapya wa Klabu ya Simba 'Simba Day'. uliochezwa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam
 Mechi ya utangulizi kati ya Simba Veterans na NMB timu hizo zilitoka sare ya 1-1
 Mashabiki wakiwa wamefurika na kusongamana kwenye geti la kuingilia uwanjani humo.
Picha ya pamoja baada ya mchezo wao wa utangulizi.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.