Habari za Punde

SIMBA YACHANUA UWANJA WA UHURU YAICHEZESHA KWATA RUVU SHOOTING 7-0

 Mshambuliaji wa Simba Emmanuel Okwi (kushoto) akishangilia moja kati ya mabao yake manne wakati wa mchezo wa Ligi Kuu Bara uliochezwa kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam,leo jioni. Katika mchezo huo Simba wameibuka na ushindi wa mabao 7-0 yaliyofungwa na Emmanue Okwi katika dakika 19, 36 na 38, Shiza Kichuya dakika ya 42 na Juma Luizio dakika ya 45 kipindi cha kwanza. Mabao mengine yalifungwa na Emmanuel Okwi tena dakika ya 52 na Erasto Nyoni dakika ya 81.

MATOKEO YA MECHI NYINGINEZO ZA LIGI KUU BARA LEO NI:
Mtibwa 1 - Stand Utd 0
Kagera Sugar 0 - Mbao Fc 1
Njombe Mji 1 - Tanzania Prisons 2
Ndanda Fc 0 - Azam Fc 1
Mwadui Fc 2 - Singida Utd 1
Mbeya City 1 - Majimaji 0
Simba SC 7 - Ruvu Shooting 0
 Mshambuliaji wa Simba Emmanuel Okwi, akifunga bao la kwanza katika dakika ya 19 baada ya kumchambua kipa wa Ruvu Shooting, Bidii Hussein (chini) wakati wa mchezo wa Ligi Kuu Bara uliochezwa kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam, leo jioni.
 Mshambuliaji wa Simba Juma Luizio, akijaribu kupiga shuti huku akizongwa na beki wa Ruvu Shooting na kipa wake Bidii Hussein,  wakati wa mchezo wa Ligi Kuu Bara uliochezwa kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam
 Okwi akijaribu kumtoka beki wa Ruvu Shooting, Shaibu Nayopa, wakati wa mchezo wa Ligi Kuu Bara uliochezwa kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam 
 Heka heka langoni kwa Ruvu Shooting
 Kichuya akitoa pasi ya mwisho.
 Erasto Nyoni akimtoka beki wa Ruvu
Okwi akishangilia moja kati ya mabao manne aliyofunga leo

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.