Habari za Punde

SINGIDA UNITED YALAMBA UDHAMINI WA SH MILIONI 250

Wachezaji wa Singida United wakiwa katika gari lao lenye nembo ya mdhamini mpya
***************************************
KLABU ya Singida United imeendelea kuneemeka baada ya kupata udhamini mnono wa milioni 250 kutoka katika Kampuni ya YARA.
Singida United ambayo imepanda Ligi Kuu ya Tanzania Bara msimu huu imepata udhamini huo mnono wa mwaka mmoja kutoka katika kampuni hiyo inayojishughulisha na kilimo cha nafaka.
akizungumza katika hafla ya kuingia mkataba iliyofanyika kwenye hoteli ya Serena, Dar es Salaam jana, Mkurugenzi wa Singida United, Festus Sanga amesema kuwa klabu yao imefurahia kuingia mkataba na YARA.
Alisema wameamua kuingia mkataba wa mwaka mmoja na kampuni hiyo kwa ajili ya kusaidia uendeeshaji wa timu hiyo.
Sanga alisema kuwa udhamini huo mpya ni habari njema za kiuchumi kwa klabu yao ambayo imefanya usajili wa 'kufa mtu' msimu huu.
“Tuna furaha kutangaza kuingia mkataba wa udhamini na YARA kwa mwaka mmoja, haya ni manufaa makubwa sana katika klabu yetu na hadi sasa tuna hekari 10 kwa ajili ya kilimo cha zao la alizeti chini ya usimamizi wa kampuni ya yara, itakayosimamia suala zima la kilimo,” alisema Sanga.
Naye mkurugenzi wa YARA, Alexandre Macedo, alisema kwamba wamefurahi kuwa sehemu ya Singida United na watayaboresha mahusiano hayo katika sekta ya kilimo.
Singida United imeendelea kuneemeka katika timu za ligi kuu hapa nchini baada ya kuingia mkataba wa udhamini kutoka katika kampuni nne ambazo ni Sportpesa, Puma, Oryx na sasa YARA.
Mkurugenzi wa Singida United, Festus Sanga kushoto akisaini mkataba pamoja na Mkurugenzi wa Kampuni ya YARA Alexander Macedo katika hafla ya kuidhamini timu hiyo ya Ligi Kuu ya Tanzania Bara.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.