Habari za Punde

TFF KUMTOA 'JELA' CHIRWA NA WENZAKE LEO?

HUKUMU ya Obrey Chirwa, Simon Msuva na Deus Kaseke inatarajiwa kutolewa kesho baada ya kamati ya nidhamu kukaa na kusikiliza na kuamua.
Wachezaji hao wanatuhumiwa kumvamia mwamuzi wakati wa mchezo wa Ligi Kuu dhidi ya Mbao FC uliochezwa Mei 20 mwaka huu hukumu yao inatarajiwa kutolewa na kamati ya nidhamu ambayo mwenyekiti wake ni Abbas Tarimba.
Akizungumza na wandishi wa habari jana,  Ofisa Habari wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) Alfred Lucas alisema watuhumiwa wote wamejulishwa kufika kwenye shauri hilo.
“Wachezaji wote wana taarifa na wanatakiwa kufika kwenye kamati kujitetea au kujibu tuhuma zinazowakabili na nashukuru Msuva naye atakuwepo kwani anatarajiwa kuwasili leo usiku (jana usiku) alisema Lucas.
Aidha Lucas alisema shauri hilo lilichelewa kusikilizwa kwani baada ya ligi kumaliza uongozi wa TFF ulikuwa katika harakati za uchaguzi mkuu uliofanyika mapema mwezi huu sasa kamati zimepatikana na zimeanza kazi
Kamati ya saa 72 iliwasimamisha wachezaji hao kutoshiriki mchezo wowote unaosimamiwa na TFF hadi tuhuma zinazowakabili.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.