Habari za Punde

TMT YAIBANA MCHENGA, BINGWA WA SPRITE BBALL KINGS KUJULIKANA JUMAMOSI

 Nahodha wa timu Mchenga BBall Stars Mohamed Yusuf akiwa anajaribu kuwatoka wachezaji wa timu ya TMT katika mchezo wa nne kati ya mitano katika fainali ya Sprite BBall Kings uliyopigwa kwenye viwanja vya Don Bosco Oysterbay Jijini Dar es Salaam. Ulimalizika kwa TMT kutoka na ushindi wa pointi 80-79.
*************************************
Na Ripota wa Blog.

Timu ya TMT imefanikiwa kurejesha furaha kwa mashabiki zake baada ya kuwafunga Mchenga BBall Stars kwa pointi 80-79 mchezo wa nne kati ya mitano katika fainali ya Sprite BBall Kings uliyopigwa kwenye viwanja vya Don Bosco Oysterbay Jijini Dar es Salaam.

TMT imefanikiwa kushinda mchezo huo wa pili kati ya minne na kuzima matumaini ya Mchenga ga kutwa ubingwa mapema baada ya kuwa tayari wakiwa wameshashinda michezo miwili kati ya mitatu.

Katika mchezo wa kwanza Mchenga walitoka na ushindi wa pointi 101- 70 za TMT, mchezo wa pili TMT wakashinda kwa pointi 82-79, na mechi ya tatu Mchenga wakashinda kwa alama 87-82 za TMT.

Kutokana na matokeo hayo timu ya TMT imeweza kusimamisha ubingwa uliokuwa unategemewa na Mchenga BBall Stars kwa siku ya juzi na kupelekea kwenda katika Game 5 siku ya Jumamosi Ijayo.

Pamoja na hayo, mechi hiyo iliweza kuonyesha utofauti na ufundi mkubwa kutokana na timu zote mbili kujifua vizuri na kusababisha kumaliza mchezo kwa tofauti ya pointi moja.

Manahodha wa timu zote mbili wamewaahidi mashabiki wao kuja kwa wingi siku ya Jumamosi kwa ajili ya kushuhudia mchezo huo wa mwisho na wenye kutoa hatma ya bingwa Sprite BBall Kings 2017 na kila mmoja akijinasibu kufanyia makosa pale walipokosea ili waweze kuondoka na kitita cha shiling milion 10.

Mchenga na TMT zitakutana tena Septemba mbili (Jumamosi) ya mwaka huu kucheza game 5 ambapo mchezo huo ndiyo utakoweza kuamua mshindi ni nani kati ya wawili hao.
Nahodha wa timu Mchenga BBall Stars Mohamed Yusuf akiwa anajaribu kumtoka nahodha wa  timu ya TMT Isihaka Masoud katika mchezo wa nne kati ya mitano katika fainali ya Sprite BBall Kings uliyopigwa kwenye viwanja vya Don Bosco Oysterbay Jijini Dar es Salaam. Ulimalizika kwa TMT kutoka na ushindi wa pointi 80-79.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.