Habari za Punde

WALLACE KARIA, RAIS NA MICHAEL WAMBURA MAKAMU NDO MABOSI WAPYA TFF

 Wallace Karia (kulia) akiapishwa na Mwanasheria wa BMT, kuwa Rais mpya wa TFF mara baada ya kutangazwa mshindi katika uchaguzi Mkuu wa Shirikisho la mpira wa miguu Tanzania TFF, uliofanyika leo kwenye Ukumbi wa Hoteli ya St. Gasper mjini Dodoma. Katika uchaguzi huo Karia aliibuka na jumla ya kura 95 akiwambwaga wapinzani wake Ally Mayay, na Richard Shija waliopata kura 9 kila mmoja, Iman Madega kura 8, Frederick Mwakalebela kura 3 na Emmanuel Kimbe kura 1.
 Michael Wambura (kulia) akiapishwa na Mwanasheria wa BMT, kuwa Rais mpya wa TFF mara baada ya kutangazwa mshindi katika uchaguzi Mkuu wa Shirikisho la mpira wa miguu Tanzania TFF, uliofanyika leo kwenye Ukumbi wa Hoteli ya St. Gasper mjini Dodoma. Katika uchaguzi huo Karia aliibuka na jumla ya kura 95 akiwambwaga wapinzani wake Ally Mayay, na Richard Shija waliopata kura 9 kila mmoja, Iman Madega kura 8, Frederick Mwakalebela kura 3 na Emmanuel Kimbe kura 1
 Rais mpya wa TFF Wallace Karia na Makamu wake, Michael Wambura, wakipongezana baada ya kutangazwa washindi katika uchaguzi huo.
************************************************
Na Ripota wa Mafoto Blog, Dodoma
Tanzania imeingia kwenye historia nyingine ya soka, na kushuhudia wajumbe wamchagua Wallace Karia na kumpa ridhaa ya kuliongoza Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) katika uchaguzi uliofanyika katika ukumbi wa Kanisa Katolikila St. Gaspar mkoani Dodoma.
Katika uchaguzi huo Karia alitwaa nafasi hiyo iliyokuwa ikishikiliwa na Jamal Malinzi, kwa kupata kura 95 akiwashinda wapinzani wake Ally Mayay na Richard Shija (kila mmoja akipata kura 9) huku Iman Madega (8), Fredrick Makalebela (3) na Emmanuel Kimbe (1) wakati wapiga kura wakiwa 128.
Akitangaza matokeo hayo leo jioni, Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi ya TFF, Revocatus Kuuli aliendelea kuweka bayana matokeo ya wagombea wa nafasi ya Makamu wa Rais, Michael Wambura alizoa kura 85 akiwaangusha Mulamu Ng’ambi (25), Mtemi Ramadhani (14) na Robert Selasela (2).
Nafasi ya wajumbe wa Kamati ya Utendaji kwa kanda namba moja ya mikoa ya Kagera na Geita, kura zilizopigwa ni 127, SaloumChama aliibuka kidedea kwa kupata kura 92 akiwatupa mbali Leopold Tasso Mukebezi (20) na Kaliro Samson (15) huku Kanda namba mbili ya mikoa ya Mara na Mwanza kura zilizopigwa ni 128 Vedastus Lufan ndiye mwakilishi wa kanda hiyo akiwaacha Eiphraim Majinge (32), George Nyanda (12) na Samuel Silas (17).
Kanda namba tatu, Shinyanga na Simiyu kura zilizopigwa ni 127 Mbasha Matutu ndiye anayeiwakilisha kanda hiyo baada ya kuzoa kura 67 akiwagaragaza Stanslaus Nyongo (42) na Bennister Lugora (18) Kanda namba nne ya Arusha na Manyara  kura zilizopigwa ni 121, Sarah Chao kura 57,Peter Temu na Omar Walii kila mmoja alipata kura 32.
Kanda namba tano ya mikoa ya Kigoma na Tabora ilibebwa na Issa Bukuku alizoa kura 80 na kuwatupa John Kadutu (29), Dk Francis Michael (12) na Abubakar Zebo (5) huku kandanamba sita ya mikoa Katavi na Rukwa imechukuliwa na Keneth Pesambili aliyepata kura 72 na kumuacha Baraka Mazengo aliyambulia kura 54.
Kanda namba saba ya Iringa na Mbeya Elias Mwanjala  alipata kura 61,Cyprian Kuyava (35)na Erick Nyamlingo (31), kanda namba nane ya Njombe na Ruvuma kura 128, James Mhagama kura 63,Vicent Majili 30,StanleyKevela 17 na Golden Sanga 16,Kanda namba tisa Lindi na Mtwara Dustan Ditopile alipata kura kura 74 huku Athumani Kambi alipata kura 54.
Kanda namba 10 Mohamed Aden alipata kura 35 akiwazidi Hussein Mwamba kura 33, Stewart Masima kura 10, Ally Suru kura 10 na George Komba kura 16 kanda namba 11 Pwani na Morogoro Francis Ndulane alitwaa kura 72, Charles Mwakambaya kura 42 na Gabriel Lucas kura 13.

Kanda namba 12 Kilimanjaro na Tanga,Khalid Abdalla alitwaa nafasi hiyo kwa kura 70 na kumuangusha Goodluck Moshi kura 55 Kanda namba 13, Lameck Nyambaya kura 41, Shaffih Dauda kura 21, Ayoub Nyenzi kura 17, Said Tully kura 10, Ramadhani Nassib kura 12,Mussa Kisoky kura 8,Saad Kawemba kura5, Ally Kamtande kura 2,Jamhuri Kihwelu kura 2, Peter Mhinzi kura moja, Emmanuel Ashery kura 1 Abdul 1
 Rais Wallace Karia akipongezwa na baadhi ya wajumbe.
 Michael Wambura akipongezwa na mmoja kati ya wajumbe
Karia akipongezwa
Baadhi ya wagombea walioangukia pua katika uchaguzi huo, kutoka (kushoto) Emmanuel Kimbe, Iman Madega, Richard Shija, Frederick Mwakalebela na Mtemi Ramadhan,wakijadili jambo baada ya kupiga kura na kupata tetesi ya matokeo. 

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.