Habari za Punde

WAZIRI MWAKYEMBE AWAPONGEZA WANAFUNZI WALIORUDI NA MEDALI RIADHA UGANDA

 WAZIRI wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe, akimpongeza Mwanafunzi wa Kidato cha tatu katika Shule ya Sekondari ya Makongo, Winifrida Makenji, aliyejizolea Medali Nne katika mashindano ya Riadha ya Shule za Afrika Mashariki yaliyomalizika hivi karibuni nchini Uganda. Dkt. Mwakyembe alikutana na wanamichezo hao walioshiriki mashindano hayo leo katika Ukumbi wa Idara ya Habari Maelezo, jijini Dar es Salaam.
 WAZIRI wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe, akizungumza na wanafunzi hao katika ukumbi wa Idara ya Habari Maelezo.
 Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe, akipokea Bendera ya Taifa kutoka kwa Nahodha wa timu ya Riadha ya Wanafunzi wa Shule za Sekondari, Davis Briton, baada ya timu hiyo kutoka kushiriki mashindano ya Shule za Afrika Mashariki yaliyomalizika hivi karibuni nchini Uganda. Dkt.Mwakyembe alikutana na wanamichezo hao walioshiriki mashindano hayo leo katika Ukumbi wa Idara ya Habari Maelezo, jijini Dar es Salaam.
Wanafunzi hao wakiwa katika mkutano huo

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.