Habari za Punde

WAZIRI MWIJAGE AWEKA WAZI MKAKATI YA VIWANDA NA MIPANGO KAZI YA JUMUIYA YA MAENDELEO KUSINI MWA AFRIKA SADC

 WAZIRI wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage, akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, leo kuhusu Mkakati wa Viwanda na mpango kazi wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Africa (SADC) baada kumalizika kwa mkutano wa 37 wa SADC uliomalizika hivi karibuni nchini Afrika ya Kusini. Kushoto kwake ni Mkurugenzi Msaidizi, Idara ya Mtangamano wa Biashara, Sekela Mwaisela na Kaimu Mkurgenzi Idara ya Uwekezaji, Aristides Mbwasi. 
 MKAKATI WA VIWANDA NA MPANGO KAZI WA JUMUIYA YA MAENDELEO KUSINI MWA AFRIKA-SADC (INDUSTRIALIZATION STRATEGY AND ROADMAP AND ACTION PLAN FOR SADC, 2015-2063)

Mkakati wa Viwanda wa SADC kwa mwaka 2015-2063 ulipitishwa mjini Harare, Zimbawe tarehe 29 Aprili, 2015, katika mkutano wa dharura wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa SADC. Mkakati huu unalenga kuzifanya nchi za SADC kuwa na uchumi wa viwanda na kushiriki zaidi katika mnyororo wa thamani kikanda na kimataifa (Regional and Global Value Chains) na hivyo kuongeza kasi ya maendeleo kwa wananchi wake.
1.1      Nguzo za Mkakati wa Viwanda
Mkakati wa kuendeleza Viwanda katika Nchi za SADC una nguzo tatu (3) zinazotegemeana ambazo ni:
(i)         Uendelezaji viwanda kama njia ya kuleta mageuzi ya kiuchumi (Industrialization as a champion of economic transformation);
(ii)        Kukuza ushindani (enhancing competitiveness); na
(iii)      Kuongeza utangamano wa kikanda.
 KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

1.2      Maeneo Makuu Yaliyoainishwa kwenye Mkakati
Mkakati umeainisha maeneo makuu (Clusters) sita (6) ambayo Nchi za SADC zinaweza kuyatumia katika kukuza ushiriki wao kwenye mnyororo wa thamani na hivyo kuongeza ushiriki wa nchi hizo kwenye masoko ya kikanda na kimataifa. Maeneo hayo ni kama ifuatavyo:
(i)         Usindikaji mazao ya Kilimo (Agro-processing);
(ii)        Shughuli zinazoendana na Uchenjuaji Madini (Minerals and mineral benefication)
(iii)      Madawa ya Binadamu (Pharmaceuticals);
(iv)      Uzalishji Bidhaa zinazotumiwa mara kwa mara (Manufacturing of Consumer Goods);
(v)        Bidhaa za Uwekezaji (Capital Goods); na
(vi)      Huduma (Services).

2.   MPANGO KAZI WA KUENDELEZA VIWANDA KATIKA NCHI ZA SADC
Mpango Kazi wa kutekeleza Mkakati wa kuendeleza Viwanda (Action Plan for implementation of SADC Industrialization Strategy and Roadmap) ulipitishwa katika mkutano usiokuwa wa kawaida wa Wakuu wa nchi na Serikali uliofanyika mwezi Machi, 2017 huko Lozitha Swaziland. Mpango kazi huo utatekelezwa katika kipindi cha miaka kumi na tano (15) kuanzia mwaka 2015 - 2030 kama awamu ya kwanza.
Mpango kazi huo umegawanyika katika maeneo makuu matano (5) ambayo yanajumuisha maeneo matatu ya kimkakati. maeneo mengine yaliyoongezwa ili kurahisisha utekelezaji wa Mkakati huo kama yafuatavyo:
(i)           Uendelezaji viwanda kama njia ya kuleta mageuzi ya kiuchumi (Industrialization as Champion of Economic Transformation);
(ii)          Kukuza ushindani (enhancing competitiveness);
(iii)        Kuongeza utangamano wa kikanda (Regional Integration);
(iv)        Masuala Mtambuka (Crosscutting issues); and
(v)          Tathmini na Ufuatialiaji (Monitoring and Evaluation).
Nchi wanachama wanawajibika moja kwa moja kwenye vipengele vinavyohusu masuala ya ndani ya nchi hususan Uandaaji wa Sera Wezeshi, Utafiti; Kuunganisha sekta ya viwanda na sekta nyingine na kuweka mazingira mazuri ya uwekezaji kwenye viwanda. Sekretariati ya SADC imekuwa na majadiliano na wahisani mbalimbali kwa ajili ya kuwaomba kuwezesha utekelezaji wa Mkakati huu. Baadhi ya Wahisani wamethibitisha kufadhili utekelezaji wa baadhi ya maeneo ya mkakati kama yafuatavyo:
(i)     Kuongeza Thamani Mazao ya Kilimo na Kuwajengea Uwezo Wajasiriamali;
(ii)    Uchenjuaji Madini na  Kuongeza Thamani Madawa ya Binadamu (Pharmaceuticals); na
(iii)  kujengea uwezo Wajasiriamali kuhusu Mpango wa Kueneza Mkakati wa kuendeleza viwanda katika Nchi za SADC.
MAENEO AMBAYO YAMEAINISHWA NCHINI TANZANIA KUWA NA FURSA KATIKA KUTEKELEZA MKAKATI VIWANDA KATIKA NCHI ZA SADC
Tathamini ya ushiriki wa nchi moja moja kwenye maeneo sita yenye fursa za kuongeza thamani (clusters) yaliyoanishwa hapo awali ilizingatia shughuli za kuongeza thamani zinazoendelea ndani ya nchi husika hivi sasa na uwezekano wa kuibua shughuli nyingine kutokana na rasilimali, sera na mazingira ya uzalishaji yaliyopo ndani ya nchi husika kwa kulinganisha na nchi nyingine za SADC.
Kufuatia vigezo hivyo, Tanzania imeainishwa kuwa na ushindani mzuri katika maeneo matano (5) kati ya sita (6) yaliyoanishwa kama yafuatavyo:
Jedwali 1: Maeneo ambayo Tanzania imeainishwa kuwa na fursa katika kutekeleza Mkakati wa kuendeleza Viwanda katika Nchi za SADC
NA
ENEO (CLUSTER)
FURSA ZA VIWANDA ZILIZOPO NA ZINAZOWEZA KUANZISHWA
1.     
Usindikaji Mazao ya Kilimo
Sukari, mihogo, bidhaa za maziwa, bidhaa za nafaka, bidhaa zinazotokana na mbegu za mafuta na bidhaa zainazotokana na misitu
2.     
Shughuli zinazoendana na uchenjuaji madini
Madini ya Chuma; base-metals (shaba, aluminium, nikeli na Kobalti); mbolea; saruji; magadi;
3.     
Madawa ya binadamu
ARV; Dawa za Malaria; Vyandarua
4.     
Uzalishaji bidhaa zinazotumiwa mara kwa mara
Bidhaa za ngozi; viatu
5.     
Utoaji huduma
Utalii
6.     
Bidhaa za uwekezaji: Mashine na vifaa
Hakuna

Manufaa kwa Tanzania yanayotokana na Mkakati huu
Tanzania itanufaika kwa kutekeleza miradi mbalimbali na hivyo kuongeza kasi ya kufikia malengo ya nchi kama ifuatavyo.

  • kushiriki katika  mnyororo wa thamani kikanda na kimataifa  (Regional and Global Value Chains) na hivyo kuongeza kasi ya maendeleo kwa wananchi wake na kuafanya Tanzania kuwa nchi ya uchumi wa viwanda; na
  • Mkakati huu utaisaidia Tanzania kushiriki na kunufaika zaidi na wigo mkubwa wa masoko ya kikanda na kimataifa.
  • Tanzania itanufaika na Transfer of Technology kutoka nchi wanachama wa SADC.
  •  Kwa kupata ufadhili Tanzania itatumia malighafi yanayopatikana humu nchini kuzalisha bidhaa zitakazoshindana katika Kanda na kukuza ushindani.
3.   MAENEO AMBAYO MKAKATI WA SADC UNAWIANA NA MKAKATI WA KUHARAKIWA UENDELEZAJI WA VIWANDA NCHINI
Mkakati wa Viwanda wa SADC unakuja katika muda muafaka kwa Tanzania, kwa vile unaendana na  Mpango wa Maendeleo wa Miaka Mitano wa nchi unayolenga Tanzania kuwa na uchumi wa Viwanda. Aidha, Mkakati huo unaendana  na Mkakati wa kuharakisha uendeleza viwanda ulioandaliwa na Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, kwenye maeneo makuu yafuatayo:
Na.
Mkakati wa Viwanda wa SADC
Mpango wa Pili wa Miaka Mitano
(i)            
Kuongeza ajira hadi asilimia 40 kufikia mwaka 2030
Ukuaji ajira utakuwa kufikia asilimia 5.4 ifikapo mwaka 2020; na katika Malengo ya  ilani ya chama cha mapinduzi ya 2015 malengo ya sekta ya Viwanda  ni kuchangia asilimia 40 ya ajira zote kufikia mwaka 2020
(ii)           
Bidhaa zinazotumiwa mara kwa mara (Manufacturing: consumer goods) wa SADC utakua kwa asilimia 30 ifikapo 2030
 Kasi ya ukuaji wa Sekta ya Viwanda  utaongezeka kwa wastani wa asilimia 10.5 ifikapo mwaka 2020
(iii)         
Unatoa kipaumbele katika Mnyororo wa Thamani na uongezaji thamani mazao ya Kilimo na yasiyokuwa ya Kilimo
Kuongeza thamani mazao yote yanayosafirishwa nje ya nchi
(iv)         
Unatekelezwa kwa kushirikisha sekta nyngine kama vile Kilimo, Madini, Uchukuzi, miundombinu, Rasilimali watu n.k. na Sekta Binafsi  imeshirikishwa kwa kuwa ndio wanaotekeleza Mkakati huo
Unatekelezwa kwa kushirikisha sekta nyingine

 TANZANIA ILIVYOJIPANGA KUTEKELEZA MKAKATI WA VIWANDA.
MIRADI AMBAYO IMESHAPATA UFADHILI NA AMBAYO INATEGEMEA KUPATA UFADHILI  KWENYE MKAKATI WA VIWANDA
     i.        Katika kutekeleza Mkakati wa Viwanda, Tanzania kupitia Sekretarieti ya SADC iliwasilisha miradi mbalimbali kuomba ufadhili, hivyo tumepata ufadhili wa kiasi cha Euro 1,400 kutoka mfuko wa  Jumuiya ya Ulaya ( European Development Fund- EDF11). Ufadhili  huo utasaidia kwenye  miradi  mine ikiwepo mradi wa kupitia upya Sera ya Viwanda( Review of Sustainable Industrial Policy-1996-2020), na kuwezesha mnyororo wa thamani wa Alizeti hususan kuimarisha masuala ya viwango na ubora(Upgrading the Tanzania Sunflowers value chain; focusing on  strengthening capacity on  SPS and standards and quality Management System. Maandalizi ya awali yameanza kama vile kuandaa activities zitazofanyika katika  kipindi cha miezi miwili ijayo.
    ii.        Mnyororo wa thamani  na kuongeza thamani kwenye mazao ya kilimo na mazao yasiyokua ya kilimo(Value chain  ana value addition on Agriculture products and non non agriculture products)

SADC Sekretarieti imeendelea kuhamasisha wafadhili mbalimbali  kufadhili miradi ya kipaumbele. Sekretarieti  inaendelea kujadiliana na International Cooperation Partners kusaidia miradi ya kipaumbele iliyoainishwa  katika mnyororo wa thamani na uongezaji thamani ya mazao ya kilimo na yasiyokua ya kilimo. Tanzania tuliwasilisha  miradi ya sekta ya ngozi na mazao yake, mbao na mazao yake na  sekta ya mavazi. Hata hivyo Secretarieti ya SADC inafanya utafiti  kuainisha Sekta ya kipaumbele kwa Kanda nzima na ripoti  ya utafiti huo utakamilika Desemba 2017.

iii) Mnyororo wa thamani kwenye sekta ya madini na Madawa (Mineral and Pharmaceutical Value Chains)
SADC Sekretarieti inatafuta  ufadhili katika  kuchenjua na kuongeza thamani Madini badala ya kusafirisha madini hayo  nje ya nchi yakiwa ghafi. Mpaka sasa zoezi la kupata wafadhili unaendelea katika ngazi ya Secretarieti ya SADC.
Kwa upande wa sekta ndogo ya madawa, Tanzania iliwasilisha miradi ya kuwezeshwa katika kuzalisha wa madawa ya magonjwa ya kuambukizwa na yasiyo ya kuambukizwa (Non communicable and communicable diseases) ili waweze kuingia katika mnyororo wa thamani na kuingia katika soko la Kikanda na Kimataifa. Sekretarieti ya SADC wanaendelea kujadiliana na Wafadhili mbalimbali kuwezesha kutekeleza Mpango Kazi wa Viwanda wa SADC

WIZARA YA VIWANDA, BIASHARA NA UWEKEZAJI

AGOSTI 2017

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.