Habari za Punde

WAZIRI NCHEMBA AFUNGUA MKUTANO WA MAJADILIANO KUHUSU WAKIMBIZI WA BURUNDI WAISHIO TANZANIA, WALIO TAYARI KUREJEA NCHINI KWAO

 Waziri wa Mambo ya Ndani, Mwigulu Nchemba, akizungumza na Wajumbe kutoka Tanzania, Burundi na Shirika la Wakimbizi katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere, jijini Dar es Salaam, leo wakati akifungua rasmi Mkutano wa 19 siku mbili wa majadiliano kuhusu Wakimbizi wa Burundi waishio nchini Tanzania, ambao baadhi wameanza kujiandikisha ili kurejea nchini kwao baada ya Rais Pierre Nkulunzinza kutangaza hali ya usalama kurejea Burundi. Mkutano huo unashirikisha Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Burundi na Shirika la Kuhudumia Wakimbizi Duniani (UNHCR), lengo ni kujadili na kuwekeana makubaliano juu ya Mpango wa Kuwarejesha Wakimbizi wa Burundi wanaohifadhiwa katika makambi ya wakimbizi ambao wako tayari kurejea nchini kwao.
  Waziri wa Mambo ya Ndani, Mwigulu Nchemba, akijadiliana jambo na Mwakilishi wa Shirika la Wakimbizi Tanzania UNHCR, Chansa Kapaya, wakati wa ufunguzi wa mkutano wa siku mbili wa majadiliano kuhusu Wakimbizi wa Burundi waishio nchini Tanzania, ambao baadhi wameanza kujiandikisha ili kurejea nchini kwao baada ya Rais Pierre Nkulunzinza kutangaza hali ya usalama kurejea Burundi. Mkutano huo ulifanyika kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam. 
 Baadhi ya Wajumbe wa mkutano huo wakimsikiliza Waziri Mwigulu
 Baadhi ya wawakilishi wa serikali ya Tanzania ndani ya mkutano huo.
Meza kuuu

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba (watano kulia), Waziri wa Mambo ya Ndani na Elimu ya Uzalendo kutoka nchini Burundi, Pascal Barandagiye,(wasita kulia), na Mwakilishi wa Shirika la Kuhudumia Wakimbizi  Duniani (UNHCR) nchini Tanzania, Chansa Kapaya (wanne kulia) wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya washiriki wa Kikao cha 19 kinachoshirikisha Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Burundi na Shirika la Kuhudumia Wakimbizi Duniani (UNHCR), lengo ni kujadili na kuwekeana makubaliano juu ya Mpango wa Kuwarejesha Wakimbizi wa Burundi wanaohifadhiwa katika makambi ya wakimbizi ambao wako tayari kurejea nchini kwao. Kikao hicho kimefanyika leo katika Ukumbi wa Mikutano wa Mwalimu Julius Nyerere, jijini Dar es Salaam

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.