Habari za Punde

YANGA YAANZA VIBAYA LIGI KUU BARA, YABANWA MBAVU NA LIPULI

Wafungaji pekee katika mchezo wa leo, mshambuliaji wa Yanga Donald Ngoma (kushoto) akiwania mpira na Seif Abdallah wa Lipuli Fc, wakati wa mchezo wa Ligi Kuu Bara uliochezwa leo jioni kwenye Uwanja wa Uhuru, jijini Dar es Salaam. Katika mchezo huo timu hizo zimetoka sare ya bao 1-1 wafungaji wakiwa ni Ngoma kwa upande wa Yanga katika dakika ya 45 na Seif kwa upande wa Lipuli (pichani) katika dakika ya 44, yote katika kipindi cha kwanza.
 Mshambuliaji wa Yanga Donald Ngoma (wa pili kushoto) akiwania mpira na Seif Abdallah wa Lipuli Fc.
 Kiungo wa Yanga, Raphael Daud, akimtoka beki wa Lipuli, Samwel Mathayo, wakati wa mchezo wa Ligi Kuu Bara uliochezwa kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam
Kiungo wa Yanga, Raphael Daud, akidhibitiwa na kipa wa Lipuli, Agathon Mkwando, baada ya kumpita beki wake, Samweli Mathayo (kulia), wakati wa mchezo wa Ligi Kuu Bara uliochezwa kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam, jioni ya leo.
 Winga wa Yanga, Yusuf Mhilu, akimiliki mpira huku akizongwa na beki wa Lipuli, Asante Kwasi,wakati wa mchezo huo.
Mhilu akimzunguka Kwasi baada ya kumpiga kanzu.
 Beki wa Lipuli akiondosha mpira huo wa hatari langoni kwake.
 Hapa Mhili sijui alikuwa akicheza ngoma gani.......
Sehemu ya mashabiki wa Yanga wakiwa wamepoa
 Donald Ngoma akijaribu kumzunguka beki wa Lipuli, Asante Kwasi.....
 Ibrahim Ajib, akipiga krosi murua langoni kwa Lipuli....
 Weka niweke........
 Shaban Zuberi wa Lipuli akimtoka Thaban Kamusoko......
 Gadiel Michael akimzunguka mchezaji wa Lipuli....
 Beki wa Yanga Andrew Vicent (Dante) akiruka kuwania mpira na Shaban Zuberi....
 Kiungo wa Yanga Papy Tshishimbi, akiruka kuwania mpira na Malimi Busungu
 Ajibu akimtoka Seme......
 Kiungo wa Yanga, Papy Tshishimbi, akijaribu kuwatoka wachezaji wa Lipuli, wakati wa mchezo wa Ligi Kuu Bara uliochezwa kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam
 Askari Polisi wakimdhibiti mwenzao aliyetaka kupigana na shabiki aliyedaiwa kumtukana askari huyo baada ya kumalizika kwa mchezo huo uwanjani hapo
 Askari huyo akiendelea kudhibitiwa na wenzake....
 Huyu naye akitaka kupigana na mwandishi wa habari mpiga picha wa East African Readio hapa akidhibitiwa na mtangazaji Tom Chilala.
 Askari wakiwa wamejazana katika mlango wa kuingilia chumba cha wachezaji wa Yanga baada ya kuzuka tafrani baada ya kumalizika kwa mchezo huo.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.