Habari za Punde

KAMPUNI YA ZOLA TANZANIA WATUA KWA KISHINDO MKOA WA DAR ES SALAAM WAZINDUA DUKA JIPYA MWENGE


Meneja Masoko wa Kampuni ya ZOLA Tanzania, Irene Mbowe (katikati) akikata utepe kuzindua Duka jipya la kuuza na kutoa huduma za ZOLA lililopo Mwenge jijini Dar es Salaam leo asubuhi, wakati wa hafla fupi ya uzinduzi huo. Kulia ni Mkuu wa kitengo cha mauzo wa ZOLA, John Amach (kushoto) ni Mkuu wa Kitengo cha Biashara wa ZOLA, Steve Kimea wakishrikiana kukata utepe kuzindua duka hilo.

Meneja Masoko wa Kampuni ya ZOLA Tanzania, Irene Mbowe (katikati) Mkuu wa kitengo cha mauzo wa ZOLA, John Amach (kulia) na Mkuu wa Kitengo cha Biashara wa ZOLA, Steven Kimea wakifurahia kwa pamoja baada ya kuzindua duka hilo. 
Muonekano wa nje ya duka hilo

Baadhi ya wafanyakazi na viongozi wa ZOLA wakiwa zibe kuandaa vipeperushi kwaajili ya wateja wao. 

Muonekano wa mtaa lililopo Duka hilo maeneo ya Mwenge nyuma ya Kituo cha daladala cha Mwenge kuelekea Tegeta.

Baadhi ya wafanyakazi wa ZOLA wakitoa maelekezo kwa wateja ya jinsi ya kutumia mashine za ZOLA.

Baadhi ya wanahabari wakipata maelezo kuhusu ZOLA

Meneja Masoko wa Kampuni ya ZOLA Tanzania, Irene Mbowe na Mkuu wa Kitengo cha Biashara wa ZOLA, Steven Kimea wakijadiliana jambo katika Laptop kabla ya kuanza afla hiyo ya uzinduzi wa Duka jipya ambalo linatoa huduma mbalimbali za umeme wa ZOLA jijini Dar es Salaam leo.

Wanahabari kazini wakati wa uzinduzi huo

Mkuu wa Kitengo cha Biashara wa ZOLA, Steven Kimea, akizungumza na waandishi wa habari baada ya uzinduzi huo
********************************************
Na Ripota wa Mafoto Blog, Dar
KAMPUNI ya Zola Tanzania leo imezindua Duka jipya kwa mkoa wa Dar es Salaam, kwa ajili ya kutoa huduma ya kuuza na kukopesha 
vifaa vinavyotumia nishati ya jua lililopo Mwenge nyuma ya Kituo cha daladala zinazoelekea Tegeta ukitokea Kituo cha Mafuta cha Puma.
Akizungumza na waandishi wa habari baada ya kuzindua duka hilo jipya, Mkuu wa kitengo cha biashara wa Kampuni ya ZOLA Tanzania, Stephen Kimea, alisema kuwa wamefungua duka hilo kwa ajili ya kuwasogezea huduma wananchi kwa kuuza na kuwakopesha vifaa hivyo vya Nishati ya Jua kwa gharama nafuu na malipo yanayochukua hadi miaka mitatu.
Aidha alisema kuwa baada ya kufungua duka hilo sasa wananchi wasio na umeme wa wa kawaida na uhakika wataweza kupata vifaa hivyo vya nishati ya jua kwa gharama nafuu.
“Madhumuni hasa ya kufungua duka hili hii leo ni kuwafikia wateja wetu wa Dar Es Salaam na Mikoa ya jirani ambayo ni Pwani na Kusini ikiwa ni moja ya mikakati yetu ya upanuzi wa maduka kama haya katika mikoa mbalimbali, pembezoni mwa Jiji pamoja na katikati ya miji lakini kwa leo tunawakaribisha wateja wetu wa Dar Es Salaam wafike eneo la Mwenge ili kupata huduma na bidhaa zetu ”, alisema Kimea.
Pia alisema kwamba wametoa huduma za sola za Zola katika vituo vya Polisi, Shule za msingi mia moja (100) pamoja na Taasisi mbalimbali za Serikali.
Bwana Kimea amewataka wananchi kuchangamkia bidhaa zao mbalimbali zinazodumu kwa muda mrefu zaidi na zenye bei nafuu zinazoendana na kipato cha Mtanzania wa kawaida, pia amewakaribisha wananchi kutembelea katika duka hilo lililofunguliwa kujionea huduma mbalimbali na uuzwaji wa vifaa hivyo kwa bei nafuu.
Mkuu huyo wa Kitengo cha Biashara wa
ZOLA, Steven Kimea, alitoa wito kwa Taasisi za Serikali ambazo hazina huduma ya umeme hasa vijijini kushirikiana nao ili kuwafikia watu wengi zaidi hasa kwenye vituo vya afya ili kuwasaidia wagojwa pamoja na kinamama wajawazito.
Kimea,alisema kuwa pindi unaponunua mtambo wa umeme wa ZOLA utatengenezewa mfumo wa umeme katika nyumba yako kwa bei nafuu na pia 
umeme wa ZOLA unaweza kutumika katika vifaa mbalimbali kama kuchaji simu, mashine za kunyolea, televisheni pamoja na kuwasha taa sita za ndani. 

Pia ukinunua vifaa vya ZOLA utapata dhamana (Warrant) ya miaka mitano endapo kifaa chochote kitaharibika mteja utatengenezewa bila gharama yeyote.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.