Habari za Punde

AZAKI ZA ZANZIBAR ZAWEZESHWA NA FCS KUFANYA MAFUNZO YA KWA VITENDO MOROGORO

 Washiriki wa mafunzo kutoka Asasi za Kiraia za Visiwani Zanzibar, wakiwa katika picha ya pamoja kabla ya kutawanyika kila kundi kuelekea katika vijiji viwili tofauti vya Msowelo na Matombo kwa ajili ya mafunzo kwa vitendo.  
 Kundi lililokuwa likielekea Msowelo likipiga picha ya pamoja mbele ya gari lao
  Kundi lililokuwa likielekea Msowelo likipiga picha ya pamoja mbele ya gari lao
  Kundi lililokuwa likielekea Matombo likipiga picha ya pamoja mbele ya gari lao
 Wakiwasili Msowelo
Na Muhidin Sufiani, Morogoro
Asasi za Kiraia kutoka Zanzibar zimewezeshwa kupata mafunzo ya siku mbili kuhusu Utetezi na Ushawishi wa Sera mkoani Morogoro. 
Katika mafunzo hayo Asasi mbalimbali kutoka Visiwani Zanzibar na Pemba zimeshiriki katika ziara hiyo ya Mafunzo iliyoratibiwa na Taasisi ya Foundation for Civil Society (FCS) chini ya mwamvuli wa Association of Non Governmental 
Organizations of Zanzibar (ANGOZA) na kuwakutanisha wawakilishi Zaidi ya 40 kutoka visiwa vya Zanzibar.
Washiriki hao walijifunza namna mashirika ya MVIWATA (Muungano wa Vikundi vya Wakulima Wadogo Tanzania) na MPLC (Morogoro Para-Legal Center) wanavyofanya kazi zao na kufikia mafaniko kwa kutoa hudua hisika kwajamii zenye matatizo ya migogoro ya ardhi.
Katika siku ya pili washiriki hao waliogawanyika katika makundi mawili tofauti walipata fursa ya kwenda katika mafunzo kwa vitendo katika Vijiji vya Msowelo na jingine likielekea Matombo, kwa mafunzo ya vitendo.
Wakiwa katika vijiji hivyo walikutana na wanaasasi wenzao na kufanya mazungumzo ili kunufaika kwa kupata maelezo ya ujuzi mbalimbali zinazofanywa na MVIWATA na MPLC. 
MVIWATA imewapeleka washiriki wilayani Kilosa katika kijiji cha Msowelo ambapo kijijini hapo kumekuwa na migogoro ya Wakulima na Wafugaji ambapo kijijini hapo MVIWATA imefanikiwa kutumia mtandao wake wa msingi kupaza sauti kwa Serikali ili kutenga maeneo ya wakulima. 
Tayari wilayani hapo kuna mashamba 9, ambayo yamefutwa na yamekabidhiwa katika mamlaka ya wilaya ili kugawiwa kwa wananchi.
Kwa upande wa MPLC yenyewe iliwaonyesha washiriki hao kazi zao katika eneo la Matombo ambako huko pia MPLC inafanya kazi 
za utetezi wa haki za umiliki wa ardhi kwa makundi mbalimbali yanayokabiliwa na changamoto hiyo. 
Aidha Shirika hilo limejizolea sifa kwa kazi zake mkoani Morogoro na pia ni shirika kongwe ambalo linafanya kazi za utetezi na ushawishi mkoani Morogoro.
Washiriki kutoka Zanzibar walitumia nafasi hiyo kubaini changamoto mbalimbali zinazoyakumba makundi mbalimbali katika 
jamii ilhali kukiwa na mapungufu katika sera na maamuzi hali inayowahitaji wananchi kufanya ushawishi na utetezi wa 
haki za kila kundi ili kuchochea jamii kubaki ikiishi kwa amani na ikiendesha maisha kwa mafanikio.
 Makamu Mwenyekiti wa Mtandao wa Msingi Msowelo, Zainab Kisegele, akizungumza na wanaasasi za Kiraia kutoka Visiwa vya Zanzibar,wakati walipofika kijijini hapo Msowelo kwa ajili ya mafunzo kwa vitendo kujifunza namna ya kupambana na changamoto za migogolo ya Ardhi na njia wanazoweza kutumia kutatua migogolo katika Kata za Vijiji.
 Mwenyekiti wa Mtandao wa Msingi Msowelo, Ally Omary, akizungumza na wanaasasi za Kiraia kutoka Visiwa vya Zanzibar,wakati walipofika kijijini hapo Msowelo kwa ajili ya mafunzo kwa vitendo kujifunza namna ya kupambana na changamoto za migogolo ya Ardhi na njia wanazoweza kutumia kutatua migogolo katika Kata za Vijiji.
 Washiri wakisikiliza kwa umakini
 Picha ya pamoja baada ya mafunzo kwa walioelekea Kijiji cha Msowelo
 Washiriki waliokuwa wakielekea Matombo wakiwa katika gari kuelekea katika mafunzo kwa vitendo.
 Wakiwa katika mafunzo
 Wakiuliza maswali kwa wenyeji wao ili kujifunza zaidi
 Mafunzo yakiendelea Matombo.....
 Mafunzo yakiendelea Matombo.....
Ushuhuda .......
Picha ya pamoja baada ya mafunzo kwa walioelekea Kijiji cha Matombo.
 Baada ya mafunzo kwa pande zote mbili Msowelo na Matombo, washiriki walikutana tena na kuungana kwa majadiliano baada ya mafunzo kwa vitendo
 
Washiriki wakijielezea jinsi walivyoweza kujifunza kutoka kwa wenzao walokokwenda.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.