Habari za Punde

DK. MERU AINEEMESHA JOTUN

Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Dk. Adelhelm Meru (watatu kutoka kulia ) akikata utepe katika ufunguzi wa kampuni kubwa Afrika Mashariki na Kati inayojishughulisha na utengenezaji wa rangi ya Jotun. Kushoto kwake ni Balozi wa Norway nchini Hanne-Marie Kaarstad.***************************************
KATIBU Mkuu wa Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Dk. Adelhelm Meru ameiahidi kampuni ya rangi ya Jotun kuwa atatoa kiwanja kwa ajili ya kutengeneza kiwanda cha rangi nchini pale watakapokuwa tayari.
Kauli hiyo imekuja baada ya kampuni hiyo kufungua duka kubwa la rangi Afrika Mashariki na kati lililopo Posta, Dar es Salaam.
Akizungumza Dar es Salaam jana, Dk. Meru amesema kuwa ujenzi wa kiwanda hicho kikubwa utasaidia kupunguza tatizo la ajira ambapo vijana wengi watapata ajira.
Alisema ujenzi wa kiwanda hicho utasaidia nchi kupata mapato kutokana na kodi ambapo pato la uchumi litaongezeka.
Dk. Meru alisema kiwanda hicho kitasaidia kuendeleza kampeni ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. John Magufuli katika Tanzania ya viwanda.
“Sisi kama serikali tunawakaribisha sana nchini Tanzania, tena mmekuta tuna sera ambazo ni rafiki kwa uwekezaji zaidi. Na habari njema ni kwamba tayari nimezungumza nao na wao wamesema wanaangalia biashara kwa miaka hii michache na baadaye wakishapata wasoko watafungua kiwanda kabisa hapa nchini,” alisema Dkt. Adelhelm.
Kampuni ya Jotun ilianzishwa nchini Norway mwaka 1926 ambapo ni moja ya kampuni zinazoongoza katika uzalishaji wa rangi duniani.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.