Habari za Punde

IBRAHIM AJIB AACHA KUMBUKUMBU UWANJA WA SABASABA NJOMBE

Mshambuliaji wa Yanga, Obrey Chirwa (kulia) akijaribu kumtoka beki wa Njombe Mji, wakati wa mchezo wa Ligi Kuu Bara uliochezwa kwenye Uwanja wa Sabasaba, mjini Njombe. Katika mchezo huo Yanga wameshinda bao 1-0 lililofungwa na Ibrahim Ajibu kwa mpira wa adhabu ndogo.
Na Ripota wa Mafoto Blog, Njombe
KIUNGO wa Mabingwa watetezi, Yanga SC, Ibrahi Ajib Migomba, leo ameandika historia mpya na pekee katika Uwanja wa Sabasaba mjini Njombe, baada ya kuisaidia timu yake kuibuka na ushindi mwembamba wa bao 1-0 dhidi ya Mji Njombe katika mchezo wao wa pili wa Ligi Kuu bara.
Ajib ameweza kuandika Historia hiyo baada ya kufunga bao pekee katika mchezo huo akifunga bao zuri na la kwanza tangu kujiunga na wana wa Jangwani na katika Ligi hii mpya iliyoanza hivi karibuni lakini pia likiwa ni bao la kwanza na kepee la aina hiyo kufungwa katika uwanja wa Sabasaba.
Njombe Mji huu ni mchezo wao wa pili wanapoteza katika uwanja wa nyumbani baada ya mchezo wa kwanza kupoteza mbele ya wana jelajela Tanzania Prisons kwa kufungwa mabao 2-1, ambapo baada ya mchezo wa leo Ibrahim Aij amewashusha hadi nafasi ya mwisho katika msimamo wa Ligi Kuu baada ya Ruvu Shooting ambao walianza kwa kipigo cha mabao 7-0 dhidi ya Simba leo wakilazimisha sare ya 1-1 dhidi ya Kagera Sugar.
Beki wa Yanga, Gadiel Michael (kulia) akimtoka mchezaji wa Njombe mji.
Yanga baada ya mchezo wa leo wamejivunia pointi tatu za kwanza katika Ligi Kuu Bara baada ya kuibuka na ushindi wa 1-0 dhidi ya wenyeji hao Njombe Mji na kufikisha jumla ya Pointi 4 na magoli mawili ya kufunga baada ya mchezo wao wa kwanza kulazimishwa sare na Lipuli wakiwa wenyeji.
Katika mchezo huo uliochezeshwa na Mwamuzi, Suleiman Kinugani wa Morogoro, aliyesaidiwa na Khalfan Sika wa Pwani na Hajji Mwalukuta wa Tanga, Hajib alifunga bao hilo dakika ya 16 kwa shuti la umbali wa mita 30 la mpira wa adhabu, baada ya yeye mwenyewe kuchezewa faulo nje ya kumi na nane.
Baada ya kupata bao hilo Yanga waliongeza kasi ya mashambulizi lakini hawakuwa na bahati ya kufunga zaidi kutokana na kushindwa kutumia vizuri nafasi walizotengeneza.
Juma Mahadhi wa Yanga, (kulia) akijaribu kumfinya beki wa Njombe Mji.
Kipindi cha pili kilibadilika kidogo na vijana wa Hassan Banyai wakaanza kuwavimbia kaka zao walio chini ya kocha Mzambia, George Lwandamina.
Sifa zimuendee kipa Mcameroon wa Yanga, Youthe Rostand aliyeokoa michomo mingi ya hatari kipindi hicho cha pili na kuinusuru timu yake kufungwa.
Katika kipindi hicho, beki wa Njombe Mji, Remmy Mbuligwe alikimbizwa hospitali baada ya kuumia kufuatia kuukalia mguu wake alipokuwa katika harakati za kuwania mpira na Juma Mahadhi.
Yanga nao walipata pigo baada ya kiungo wake Mzimbabwe, Thabani Kamusoko katika dakika ya 49, aliumia na kushindwa kuendelea na mchezo, nafasi yake ikachukuliwa na Raphael Daudi.

MATOKEO YA MECHI NYINGINE ZA LEO NI:-
Kagera Sugar 1 - Ruvu Shooting 1
Singida Utd 2 - Mbao Fc 1
Mtibwa Sugar 1 - Mwadui Fc 0
Mbeya City 0 - Ndanda Fc 1
Njombe Mji 0 - Yanga 1

Stand Utd 0 Lipuli 1

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.