Habari za Punde

MABOMU YA MACHOZI, YATUMIKA KUWATAWANYA MADIWANI WALIOANDAMANA KUSHINIKIZA MGODI KULIPA KIASI CHA DOLA ZA KIMAREKANI MILIONI 12.65

Baadhi ya askari wa kikosi cha kutuliza Ghasia wakiwa kwenye Barabara inayotoka Mgodi wa Dhahabu wa Geita GGM wakati walipokuwa wakiwatawanya wafanyakazi wa Kampuni hiyo waliokuwa wamefunga njia ya kuzuia magari kuingia na kutoka mgodini hapo. Maandamano hayo yaliongozwa na wafanyakazi pamoja na wananchi wa mji huo.
Wananchi na Madiwani wakiwa katikati ya barabara hiyo wakiwa wamepanga mawe kabla ya kuanza kutawanywa.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Geita, Elisha Lupuga, akizungumza katika kikao akielezea nia ya maandamano yao na jinsi walivyotawanywa na polisi.
Mkuu wa Wilaya ya Geita Mwl, Herman Kapufi, akizungumza na waandishi wa habari baada ya wananchi hao kutawanywa na askari.
Baadhi ya wajumbe wa kikao hicho wakimsikiliza Mkuu wa Wilaya.
Mkuu wa Mkoa wa Geita Meja Jenerali Mstaafu Ezekiel Kyunga, aliwataka wananchi kutulia na kusubiri meza ya mazungumzo na Naibu waziri wa Nishati na madini siku ya Jumatatu.
Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoani Geita Mponjoli Mwabulambo, akizungumza. Picha na Maduka
******************************
Jeshi la Polisi Mkoani Geita limelazimika kutumia mabomu ya
machozi na kupiga risasi za moto hewani kuwatawanya waandamanaji
ambao walikuwa wakiongozwa na Madiwani wa Halmashauri mbili za mji na
Wilaya ya Geita waliokuwa wamefunga barabara ya mgodi huo kuzuia
magari kuingia na kutoka katika Kampuni ya uchimbaji madini ya dhahabu ya Geita (GGM), kushinikiza kulipwa 
deni wanaloidai GGM kiasi cha zaidi ya Dola Bilioni 12.65.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.